Featured

    Featured Posts

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AENDA SINGAPORE LEO, NI KATIKA MKUTANO WA JUKWAA LA LA KIUCHUMI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpangoleo ameondoka nchini jana Novemba 14, 2021 kwenda  Sentosa Island Nchini Singapore kushiriki mkutano wa siku tatu wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021, ambao unaaza leo hadi Novemba 19, 2021.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Mkutano huo una lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo muelekeo mpya wa kiuchumi baada ya athari za Uviko19.

"Aidha Makamu wa Rais anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Viongozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wafanyabiashara pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo pamoja naTaasisi zao", imesema taarifa hiyo.

Makamu wa Rais Dk. Mpango
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana