Featured

    Featured Posts

SIMBA YAICHARAZA RED ARROWS YA ZAMBIA TATU BILA, JIJINI DAR ES SALAAM

CCM Blog, Dar es Salaam

Timu ya Simba Sc imefanikiwa kuwachapa Red Arrows Fc ya  Zambia kwa mabao 3-0, katika mchezo uliopigwa leo katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Simba walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa wanaongoza kwa mabao mawili yaliyofungwa na Benard Morrison na Meddie Kagere.

Simba ilipata bao la tatu katika dakika 79 ya kipindi cha pili, kupitia tena kwa nyota wao Benard Morrison, na kufuatia ushindi huo Simba inahitaji ushindi wowote au sare katika mchezo ujao ili waweze kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho ambapo Red Arrows watakuwa nyumbani kwenye mchezo huo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana