Na Jastini Cosmas, Kigoma
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma kimeonya kuwa hakitawavumilia viongozi wanaotengeneza makundi ndani ya chama, kitendo ambacho kina sababisha mpasuko na kuleta utengano ambao hautakiwi ndani ya chama.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Malima Mobutu katika mkutano wa Halmashauli Kuu ya CCM mkoa wa Kigoma ambapo ameeleza kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chama wanatengeneza makundi kitendo ambacho kina sababisha utendaji kazi kuzorota.
Mobutu amekea t na kuonya kuwa kuwa kiongozi atakayebainika akifanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili uwe mfano kwa viongozi wengine wanaotengeneza makundi ya aina hiyo.
Wakati huo huo Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kigoma imeridhishwa na usimamizi wa fedha katika utekelezaji wa miradi mbali mbali mkoani hapa na kumtunuku cheti cha pongezi Mkuu wa Mkoa Kigoma Thobiasi Andengenye kwa kusimamia vizuri ilani ya CCM.
Kwa upande wake Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa ilani ya CCM itaendelea kutekelezwa kwa asilimia zote na kuwachukulia hatua wanao hujumu miradi ya wanchi.
Ameongeza kuwa kuna wizi umeibuka wa kuiba mafuta na nondo katika miradi ya ujenzi wa barabra za kiwango cha lami zinazojengwa katika mkoa wa Kigoma kitendo ambacho kinasabaisha miradi hiyo kutoisha kwa wakati na kuonya kuwa atakaye bainika akihusika na wizi huo hatua kali za kisheria zitachukurwa dhidi yake.
Post a Comment