Featured

    Featured Posts

BUTONDO AISHUKURU SERIKALI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KISHAPU+video

Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniface Butondo amempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Naibu wake, Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa uchapakazi wao lakini pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kwa kutenga fedha ya miradi ya maji katika Jimbo la Kishapu. Ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kutiliana saini mikataba kati ya Mkandarasi atakayejenga mradi wa maji Kishapu, Kampuni ya Emirates na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mijini na Vijijini (RUWASA) Februari 11, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Mhandisi Clement Kivegalo  akitiliana saini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Emirates, Deogratius Marandu kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika Jimbo la Kishapu, Shinyanga.
Mhandisi Kivegalo akibadilishana hati ya mkataba na Marandu wa Emirates,

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akihutubia wakati wa hafla hiyo na kuwaomba mameneja wa Maji wa Mikoa kusimamia vizuri miradi hiyo.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca  Mahundi akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Butondo akiwa na wabunge wenzake wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya mameneja wa maji wa mikoa na wakandarasi wakiwa katika hafla hiyo.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Butondo akitoa shukrani na pongezi hizo....
 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana