Featured

    Featured Posts

MBUNGE MWAKANG’ATA AIBANA SERIKALI INA MPANGO GANI WA KUENDESHA MAFUNZO KWA WANAWAKE KABLA KUKOPESHWA?+video

 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata amehoji mpango wa serikali wa kuongeza mkopo wa asilimia 10 wa halmashauri kwa vikundi vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu utokanao na mapato ya halmashauri hiz pamoja na kuwapatia mafunyo kabla za kuwakopesha.


Mwakang’ata amesema vikundi vingi vinavyopata mikopo hiyo kutoka katika halmashauri zao bado havijanufaika na mkopo huyo kutokana na kiwango kidogo cha fedha wanachopatiwa.

”Wanawake au vikundi wanapopata mkopo wanapata kwa kiwango kidogo sana kiasi kwamba haiwasaidii hivyo kuna mpango gani wa kuwaongeza?”


Aidha Mwakang’ata amehoji mkakati wa serikali wa kutoa elimu ya mikopo hiyo kwa wajasirimali ikiwepo elimu ya ujasiriamali kabla ya kuwakabidhi mkopo ili iweze kuwa na manufaa kwao.

“Serikali inampango gani wa kuwajengea mafunzo na uwezo wanaokopa kabla hawajapata mkopo huo”


Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema kwa sasa serikali haijaweka mpango wa kuongeza asilimia ya mkopo hio, aidha serikali inafanya tathmini ya kina ili kubaini mafanikio na changamoto zilizopo ili kuchukua hatua stahiki kwa mikopo hiyo.


Dkt. Dugange amesema wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wanakopeshwa asilimia 10 kwa maana ya 4, 4, 2  kwa makundi hayo bila kuwa na kiwango halisi cha ukopeshwaji kutegemeana na aina ya kikundi na shughuli zao.


Dkt. Dugange amesema serikali imetoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatoa fedha zenye tija badala ya kutoa fedha kidogo kwa vikundi ili mkopo huo uweze kuwa na tija kiuchumi. 


Katika hatua nyingine Waziri Dugange amesema serikali kupitia maafisa maendeleo nchini wameweka mpango mzuri wa mafunzo  wa kuwajengea uwezo na kuwatembelea kuhakikisha kuwa wanafanya biashara zao.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana