Na Bashir Nkoromo, Dodoma
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi imemteua Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana kugombea Umakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, kuchukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara MMzee Philip Mangula ambaye ameng'atuka.
Kinana ameteuliwa na Vikao vya Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) vilivyofanyika leo Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan na inatarajiwa atachaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika kesho katika ukumbi wa Jakaya Kikwete pia jijini Dodoma.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara uya Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema leo kwamba Kinana amepotishwa na vikao hivyo baada ya kupokwa barua ya Mzee Mangula aliyomwandikia Mwenyekiti wa CCM Rais Samia, kuomba kung'atuka.
Mzee Mangula ambaye alihudumu Umakamu Mwenyekiti wa CCM Bara tangu mwaka 1912, ameomba kung'atuka ikiwa leo pia ndiyo siku yake ya kuzaliwa ambapo sasa ana umri wa miaka 80.
Shaka amesema pamoja na mambo mengine, katika Vikao hivyo Halmashauri Kuu ya CCM imewasamehe na kumrejesha kuwa mwanachama wa CCM Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa zamani Bernard Membe na aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Jang'ombe Abdallah Maulid.
Amesema Membe na Maulidi warejeshewa uanachama wao kufuatia kukikomba radhi Chama Cha Mapinduzi mara tatu na wamerejeshwa kwa mujibu wa kanuni na Katiba ya CCM, na kwamba taratibu za kupewa kadi za uanachama zitafanyika katika maeneo yao.
Post a Comment