Featured

    Featured Posts

KANISA HALISI: KUMUOMBEA MEMA RAIS SAMIA SIYO HIARI NI AGIZO LA MUNGU BABA, IBADA YA KUPOKEA 'NAMBA MOJA' KUFANYIKA NJOMBE

Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Kanisa Halisi la Mungu Baba limesema suala la kumuinua (kumuombea) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan siyo la hiari bali ni la lazima kwa kuwa ni agizo la Mungu Baba kwa kila anayemtii na kumuabudu kwa haki.

Hayo yamesemwa leo na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Baba Halisi, katika Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga Jijini  Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya Uzao (waumini).

"Kumuombea Rais wa nchi katika ibada siyo jambo la hiari, bali ni kutekeleza agizo la Mungu Baba, Nataka mnielewe, sina upendeleo, yaani siyo kwamba najipendekeza ni 'sauti', hata kesho ukiwa wewe tunakuombea, ili mradi uwe umekuwa Rais kwa haki", alisema Baba Halisi, huku akionyesha kutabasamu mbele ya uzao (waumini).

"Wakati tunaomba Taifa letu liendelee kuwa na amani na utulivu na upendo mmoja usiobagua, basi tumuombee Rais wa Taifa letu Samia Suluhu Hassani, mabaya yote yasimwelekee, madongo, mashimo, makorongo wanayomuwekea barabarani yafutike.

Rais Samia aendelee kujawa na hekima na maarifa ya kuliongoza Taifa hili kama Mungu Baba mwenyewe alivyomkusudia", akasema Baba Halisi wakati akimuombea Rais Samia na kuendelea kuwaombea walio chini yake, akiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa mikoa, Wilaya na viongozi wote hadi wa ngazi za chini.

Maombi hayo ya kumuinua Rais Samia yalienda Sanjari na upokeaji matunda (Sadaka) ya Chanzo Halisi na baadaye Baba Halisi alitangaza rasmi kwamba wiki hii atakuwa mkoani Njombea kuendesha Ibada kubwa ya kupokea 'Namba Moja'.

"Wiki hii tutakuwa Njombe, tunaenda kupokea Namba Moja, Kama unataka Kampuni yako iwe namba moja, au unataka Shughuli yako yoyote iwe namba moja twende", alisema Baba Halisi akiwaambia Uzao (waumini) kwenye Ibada hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saimia Suluhu Hassan.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana