Featured

    Featured Posts

KANISA HALISI LA MUNGU BABA JUMAPILI HII KUFANYA MKUTANO WA MAOMBI NA MAOMBEZI MJINI NJOMBE, KUWAPONGEZA PIA KINGS FM KWA KUINUA NYIMBO ZA INJILI

Na CCM Blog, Dar es Salaam
Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, Jumapili hii litakuwa na Mkutano wa Ibada ya Maombi na Maombezi utakaofanyika katika Viwanja vya Turbo Njombe mjini.

Taarifa iliyopatikana kutoka Kanisa Halisi la Mungu Baba Kituo cha Njombe, zimesema, Maombi hayo yataongozwa na Kiongozo Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi na kuhudhuriwa na baadhi ya Makuhani na Uzao (waumini) wa Kanisa hilo.

Katika Ibada hiyo ya Maombi na Maombezi, Baba Halisi atatumia nafasi hiyo pia kutoa pongezi kwa Kituo cha Redio cha Kings FM kilichopo katika mkoa huo wa Njombe kwa kuinua na kukuza nyimbo za kumtukuza Mungu Baba kwa kuanzisha kipindi cha 'Gospal Sunday'.

Taarifa zimesema katika kipindi hicho cha Gospel Sunday cha kila siku ya Jumpili, Radio hiyo hupiga nyimbo mbalimbali za Injili kwa ajili ya kutangaza na kukuza nyimbo hizo na Waimbaji wake, hususan zinazoimbwa na waimbaji wa nyanda za juu Kusini.

Katika jitihada hizo za kutangaza na kukuza nyimbo hizo za Injili na waimbaji wake, katika kipindi hicho cha Gospel Sunday Radio hiyo imeweka  pia kipengele cha 'Top 5' yaani tano bora ya nyimbo hizo za Injili zinazokuwa zinapigwa.

Taarifa zimesema kufuatia kipengele hicho cha Top 5, hivi karibuni wimbo wa Bendi ya Muziki wa kumtukuza Mungu ya Kanisa Halisi la Mungu Baba, wa 'Habari Njema' uliweza kudumu katika nafasi ya kwanza ya tano bora kwa majuma mawili mfululuzo tukio ambalo Kanisa Halisi limelipokea kwa mtazamo wa baraka kubwa.

Kings  FM ambayo ni maarufu katika mkoa wa Njombe, husikika pia katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Iringa, na Songwe.

Wanamuziki wa Bendi ya Kanisa Halisi la Mungu Baba ya Muziki wa kumtuza Mungu Baba wakiimba wakati wa Ibada ya Jumapili iliyofanyika jana, Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam.

 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana