Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu, Tegeta, Namanga Jijini Dar es Salaam, Jumapili hii, litapokea pongezi maalum kutoka Kituo cha Radio ya Kings FM ya mkoani Njombea, kufuatia wimbo wa Bendi yake ya muziki wa kumtukuza Mungu wa 'Habari Njema' kushika namba moja katika nyimbo za Injili zilizoshindanishwa na kituo hicho, hivi karibuni.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Baba Halisi amesema, pamoja na yeye mwenyewe, na baadhi ya Makuhani na Uzao (waumini) wa Kanisa hilo kwenda kupokea 'Namba Moja' hiyo ya Wimbo wao, pia Bendi ya Kanisa hilo itakwenda mjini Njombe kutumbuiza kwenye hafla hiyo ya aina yake.
"Kituo cha Radio cha Kings FM cha Njombe kiliamua kushindanisha nyimbo za Kanisa Halisi la Mungu Baba na nyimbo mbalimbali nyingine za Injili bila sisi wenyewe (Kanisa Halisi) kujua, nyimbo za Kanisa Halisi hasa wimbo unaoitwa 'habari Njema' ukapata namba moja, hicho ndicho tunachenda kupokea", Baba Halisi alisema jana, kumwambia Mwandishi wa habari hii.
Kituo cha Radio cha Kings FM, ni kituo cha Radio ni maarufu mkoani Njombe ambacho mbali na kusikika katika maeneo yote ya mkoa huo wa Njombea pia kinasikika katika maeneo karibu yote katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe na Ruvuma.
Post a Comment