Featured

    Featured Posts

MATUKIO YA AG DK. FELESHI KATIKA PICHA, IKIWEMO KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani  Nchini Tanzania,  Mhe. Donald Wright wakati Balozi huyo alipomtembelea Mhe. Mwanasheria Mkuu wa  Serikali Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya masuala  waliyozungumza  na kubadilishana  mawazo ni pamoja na suala  la Biashara Haramu  ya Usafirishaji wa Binadamu.
Mmoja wa  wageni waalikwa  akiteta jambo na Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi wakati wa hafla ya  uzinduzi wa  Kituo   cha  Kikanda cha Kupambana na Ugaidi (The Sourthen African Development Community Regional  Counter Terrorism Center) ( SADC- RCTC) Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ilifanyika Jijini Dar Es Salaam mwanazoni mwa wiki hii .
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt, Eliezer Feleshi akiwa  katika picha  ya pamoja  mara ya baada ya  mazungumzo na  Mtendaji Mkuu wa  Benki ya  Standard  Chartered Tanzania  Bw. Sunjay Rughani aliyefuatana na  Bw, Walarick Nittu  Mwanasheria na Katibu wa Benki hiyo. Bw. Rughani alimtembelea  Mhe. AG ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Mhe Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akiagana na   Bw. Kadari Singo Mtendaji   Mkuu wa  Uongozi Institute.  Bw. Singo na Ujumbe wake walifika  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mtumba, Dodoma na kisha kuwa na  mazungumzo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana