MPANGO wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), umeendesha mafunzo ya uelewa juu ya urasimishaji rasilimali kwa maofisa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma Machi 21,2022. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo yaliendeshwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mkurabita, Glory Mbilimonyo pamoja na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa mpango huo, Anthony Temu.
Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa mpango huo, Anthony Temu (kulia) akipitia baadhi ya nyaraka wakati wa mafunzo hayo.Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, Joyce Manyanda akitoa pongezi na shukrani kwa MKURABITA kufanikisha mafunzo hayo.
Baadhi ya wakuu wa Idara wa Halmashauri hiyo wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, maafisa hao wa MKURABITA, Mbilimonyo na Temu wakiendesha mafunzo hayo huku Kaimu Mkurugenzi Manyanda akitoa shukrani na pongezi kwa MKURABITA...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment