Kahama, Shinyanga
Katibu Mkuu UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi, Machi 19, 2022 aliongoza Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwemyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Kahama, Shinyanga.
Katika Maadhimisho hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, alipiga simu kuzungumza na vijana katika kongamano la kuadhimisha mwaka mmoja wa Kishindo wa Serikali ya Awamu ya sita kupitia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana ndugu Kenani Kihongosi
Amewapongeza na kuwashukuru vijana kwa mchango wao katika siku 365 za Serikali ya awamu ya sita na kuwasisitiza juu ya kulinda Amani na utulivu.
"Niwaombe sana tuendelee kulinda Amani na utulivu, tuchape kazi, tufanye siasa za kistaarabu. Vijana ninyi ndio nguzo yangu nawategemea sana"
Kongamano hilo limefanyika Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama, Jumuiya na Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mh Festo Kiwaga, Wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM TAIFA, Wenyeviti na Makatibu wa Chama na Jumuiya.
#KaziIendelee
Post a Comment