Featured

    Featured Posts

MKUU WA MKOA RUVUMA MGENI RASMI MATEMBEZI YA KUHAMASISHA AFYA YA KINYWA NA MENO

  Maandalizi Chama cha Wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno (TDA)  kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya afya ya Kinywa na Meno Tanzania na kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kinywa na Meno Duniani (WOHD) Machi 20, 2022.

Kitaifa maadhimisho haya yatafanyika katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. Mgeni rasmi katika Matembezi ya kuhamasisha afya ya Kinywa na Meno anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Ruvuma Brigedia.Jen Wilbert Ibuge.


 kaulimbiu ni: JIVUNIE KINYWA CHAKO KWA USTAWI WA AFYA YAKO. 


Mgeni rasmi katika kilele cha  Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi  

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Chama hicho Dkt. Gustav Rwekaza leo Machi 11, 2022, wakati alipokuwa akizungumza na Wanahabari (pichani hawapo) katika Ofisi ya chama hicho  na pia anawakaribisha  Wananchi wote wakazi wa Mkoa huo na Vijiji jirani  kupata huduma bila malipo na huduma hizo ni: 


 Uchunguzi wa Kinywa na Meno kwenye Halmashauri (5) kati ya (8), Matibabu ya Kinywa na meno,  Elimu ya afya ya Kinywa na Meno bure,


Uchunguzi na matibabu kwa  Watoto wenye Mahitaji Maalum na Huduma za Kinywa na Meno kwa Mama Wajawazito na Watoto (RCH).


Pia Anawashukuru wadau kwa ushirikiano katika maandalizi ya siku hii muhimu kwa ustawi wa afya za watanzania.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana