Featured

    Featured Posts

RC MTAKA AUMALIZA MGOGORO WA ARDHI BAHI ULIOFIKA HADI KWA RAIS+video

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akihitimisha mgogoro wa ardhi wa muda mrefu uliozuka kati wananchi Bahi Mjini, Kata ya Mbamatwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambao pia ulitinga kwa Rais Ikulu ya Dodoma. RC Mtaka ameumaliza mgogoro huo kwa kuzikutanisha pande hizo tatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbamatwa Machi 7, 2022 ambapo kila upande ulipewa wasaa wa kujieleza na baadhi kutoa ushahidi na vithibitisho.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda naye akisema maneno ya kuhitimisha mgogoro huo wa muda mrefu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bahi, Jamila Mujungu  akishiriki katika usuluhishi wa mgogoro huo na kuomba busara itumike kwa pande zote  ikiwemo kuwapatia sehemu ya viwanja wananchi 48 waliomo kwenye mgogoro huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bahi,Stewart Masima naye akishiriki katika suluhu ya mgogoro huo.
Diwani wa Kata ya Mbamatwa akielezea historia ya mgogoro huo.
Diwani wa Kata ya Bahi akelezea kuhusu mgogoro huo.
Baadhi ya wakazi wa Bahi Sokoni walioathirika na mgogoro huo.
Mmoja wa waathirika wa mgogoro huo akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa  Mtaka na kuomba atumie busara kuumaliza mgogoro ili kila upande upate haki.
Boaz ambaye alidaiwa kuandika barua kwa rais kuhusu mgogoro huo, akikana kuandika barua hiyo.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mbamatwa akielezea kwa masikitiko jinsi ardhi yao ilivyotwaliwa bila kushirikishwa na kuomba Serikali iwarejeshee


Sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.




 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue namna mgogoro huo ulivyomalizwa.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana