Featured

    Featured Posts

AG DK. FELESHI: KUNA HAJA YA KUWEPO VITUO VYA KUTOA HUDUMA YA PAMOJA VYA KUSHUGHULIKIA MATUKIO YA UBAKAJI NA UNYANYASAJI WA KINGONO

Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji  Dk. Eliezer Feleshi amesema kuna haja na umuhimu wa kuwa na vituo vya kutoa huduma ya pamoja ( One Stop Center) kwa waahiriwa wa matukio ya ubakaji na uyanyasaji wa kingono.

AG Jaji Dk. Feleshi ametoa ushauri huo mwishoni  mwa wiki alipokutana na kufanya  mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Legal Service Facility (LSF)  Lulu Ng’wanakilala, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Amesema uwepo wa vituo hivyo si tu utaongeza kasi ya kushugulikia matukio hayo lakini pia utaharakisha upatikanaji wa haki kwa wakati na kutoa ahueni kwa waathiriwa wa matukio hayo.

AG Jaji Feleshi ameishauri Taasisi hiyo ya  LSF ambayo ni mdau  muhumu kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na wadau wengine nje ya Serikali kwa kile alichosema kwa sababu  wao  tayari wanazo pragramu  kadhaa wanazoshirikiana na  Serikali.

 Aametolea mfano  wa  Nchi ya Afrika Kusini ambayo imeazisha vituo kama hivyo vinavyojulikana kama  Thuthuzela Care Center na kwamba uwepo wa vituo hivyo ambavyo vimesambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo umerahisisha sana ushughulikiaji wa matukio hayo na utoaji wa haki kwa wakati.
 
Akifafanua zaidi  kuhusu  vituo hivyo , AG jaji Feleshi, amesema vituo hivyo vitatakiwa kuwa na watoa huduma  wenye utaalamu na weledi wa kushughulikia visa hivyo.

“Vituo hivi vinatakiwa kuwa na daktari, Polisi, mpelelezi, Mwendesha Mashtaka, Afisa Ustawi wa Iamii, Wataalamu wa  Saikolojia na  Ushauri Nasaha pamoja na wadau wengine.

Inatakiwa muathiwa aliye nyanyaswa kingono au kubakwa anapofika kituoni hapo anapate huduma zote  hapo hapo, kama daktari anakuwapo, kama mpelelezi yupo, kama mwendesha mashataka anakuwapo na polisi anakuwapo”. Anabainisha AG Jaji Feleshi.
 
AG Jaji Feleshi amebainisha  kwamba, kwa uzoefu wake akiwa  Mwendesha Mashtaka wa Serikali lakini pia kama Jaji amekuwa akishughulikia kesi za ubakaji na unyanyasi na kushuhudia mashauri mengi kutofikia tamati kutoka na sababu nyingi zikiwamo za upepelezi na ushahidi kuvurugwa.

“Wakati mwingine unaona kabisa hapa  kuna kesi ya kujibu na haki inatakiwa kutendeka lakini mara unakuta mpelelezi anashindwa kuifanya kazi yake ipasavyo au  ndugu wa  muathiwa wanaingilia kati kwa kutaka   wayamalize  kifamilia, kimilia au kwa kuficha ushahidi na hata kumrubuni muathiwa", Amebainisha AG Jaji Feleshi.

Akasema, jambo lingine linachangia kutopatikana kwa ushahidi wa kumtia mtuhumiwa hatiani ni kwa waathiriwa kutoenda Polisi mapema baada ya tukio au  wanakwenda Polisi wakati ushahidi  umeshavurugwa.

“Sheria inataka muathiwa anapofanyiwa uovu huo aende mara moja Kituo cha Polisi au Kituo cha matibabu, lakini  hali ilivyo ama waathika wengi wanaficha uovu huo kwa sababu mbalimbali  au wanakwenda kutoa taarifa wakati ushahidi umeshavurugwa, Napenda kusisitiza kwamba, kuficha kosa ni  kosa kisheria” amesisitiza.

Anasema matukio ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono ni 'very technical' katika kuyashughulikia kutoka na  mazingira na unyeti wa matuko  yenyewe na ndiyo maana uwepo wa vituo hivi utasaidia sana kwa sababu wataalamu wote watakuwa mahali pamoja.

AG Jaji Feleshi amesema pamoja na uwepo wa madawati ya jinsia katika vituo vya Polisi na uwepo wa mashirikia yasiyo ya kiserikali  yanoshughulia  matukio hayo bado  jitihada zaidi zinahitajika.
 
Akasema   Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya  Mashtaka tayari yana Divisheni zinazoshughulika na masuala ya Uratibu hivyo  Ofisi hizo mbili zitakuwa tayari kutoa ushirikiano  katika  jambo hilo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi  huyo wa  LSF amemshukukuru Mwanasheria Mkuu kwa wazo hilo na kwamba watalifanyia kazi na kwamba Taasisi hiyo itaendelea  kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika utoaji wa msaada wa kisheria  pamoja na kuwaelimisha na kuwawezesha wadau wao hususani  wanawake kuhusu masuala yahusuyo sheria pamoja na kutambua haki zao.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk. Eliezer Feleshi akiwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility. Lulu Ng'wanakilala, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika  mwishoni mwa  wiki ofisni kwake Jijini Dar  es Salaam. (Na Mpihapicha Maalum)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana