Featured

    Featured Posts

TAASISI YA DEO MWANYIKA YAANZISHWA KUPINGA UKATILI DHIDI YA MWANAMKE NA MTOTO

 


Mbunge wa Njombe Mjini, Deo Mwanyika akitangaza kuanzisha  Taasisi ya Deo Mwanyika Foundation itakayojihusisha na  kupinga ukatili kwa Mwanamke na Mtoto

                       

Katika kupinga vitendo vya ukatili mkoani Njombe Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deo Mwanyika amesema kuwa yuko mbioni kufungua Taasisi ya kupinga ukatili kwa Mwanamke na Mtoto huku akisema Taasisi hiyo inaitwa Deo Mwanyika Foundation na nitafanya kazi kwa Ukaribu na Wanawake.

"Taasisi hii ya Deo Mwanyika Foundation itafanya kazi kwa Ukaribu na Wanawake kwani hawa ndio watu muhimu katika kupinga ukatili kwa Mwanamke na Watoto maana ndani ya Jamii kuna ukatili unafanyika na pengine  hauripotiwi kabisa" @DeoMwanyikaMbungeNjombeMjini.

"Nawapongeza sana Wanawake kwa Siku yenu hii Muhimu maaana Wanawake Mnamchango mkubwa sana  kwa Taifa na Jamii,Mimi Mbunge wenu Mwenyewe Nipo hapa kwaajiri ya Mwanamke kwa maana ya Mama yangu, Mke Wangu,na Watoto wangu" amesema wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa Njombe Mjini Machi 8, 2022.




 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana