"Nimeona ni busara kutoa maelekezo ya kuanzishwa kwa makongamano ya wadau wa elimu katika kata zote 28 zenye jumla ya vijiji 101 katika majimbo yote mawili ya singida mashariki na singida magharibi katika wilaya ya Ikungi.
Lengo la makongamano haya ni kuwaleta pamoja wadau wa elimu katika ngazi ya kata ambao watajadili kwa mapana changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kati ngazi ya kata pamoja na fursa katika sekta ya elimu katika ngazi ya kata
Hapa tutafanikiwa kwanza kupata maoni ya wadau katika ngazi ya kata, lakini pia ziko changamoto ndogo ambazo zitaweza kutatuliwa katika ngazi ya kata mfano masuala ya mdondoko wa wanafunzi mashuleni unaosababishwa na utoro na wanafunzi kupewa mimba,changamoto za walimu kufundisha kwa kutozingatia mitaala, na matumizi mabaya ya rasilimali za shule mfano ardhi ambayo wanaweza kuiwekea mpango mzuri wakailima kwa manufaa
Kwangu mimi naamini kwa mtandao mzuri wa kiuongozi katika ngazi ya kata ambao unawajumuisha mtendaji wa kata, afisa elimu kata, diwani, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, watendaji wa vijiji, walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari za umma na binafsi zilizopo katika kata na wadau wengine mfano wawekezaji wenye makampuni na biashara wakija pamoja naamini ziko changamoto zitatatuliwa
Tumefanya majaribio kwa awamu mbili ya kuwa na kongamano la wadau wa elimu katika kata ya issuna na kongamano limefanikiwa kwa kiasi kikubwa hivyo nimeona sasa ni wakati sahihi wa jambo hili kwenda kata zote, na maafisa tarafa kwa kushirikiana na watendaji wa kata na maafisa elimu kata wataratibu jambo hili kwa uweledi mkubwa.
Naamini sana katika jitihada za pamoja kuanzia ngazi ya kijiji na kata na kila mtu akitimiza wajibu wake tunaweza kuwa na msingi mzuri sana wa elimu katika wilaya yetu ya ikungi, ifike sehemu hata tuweze kutoa motisha ndogo ya zawadi kwa walimu wetu katika ngazi ya kata".
#IkungiYetu #ElimuYetu #UbunifuWetu
Post a Comment