Lumumba, Dar es Salaam, leo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amekutana na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald Wright, na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi hiyo ya Marekani.
“Mazungumzo yetu yalikuwa ya kawaida, tumezungumzia namna ya kuimarisha uhusiano pamoja na ustawi wa wananchi,” amesma Kanali Mstaafu Kinana, akizungumza baada ya balozi huyo kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Aprili 11, 2022.
Amesema miongoni mwa maeneo waliyoyagusia katika mazungumzo yao ni pamoja na kuimarisha huduma za kijamii ikiwamo afya na utoaji haki kupitia mifumo mbalimbali.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald Wright, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiagana na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald Wright, baada ya mazungumzo hayo, leo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akimsukuru Balozi wa Marekani hapa nchini Donald Wright, baada ya mazungumzo yao, Ofisi Ndogo ya makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo. Picha: Fahadi Siraji
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment