Featured

    Featured Posts

WAZIRI NAPE AANZA ZIARA YA KUKAGUA NA KUHAMASISHA UTEKELEZAJI WA ANUANI ZA MAKAZI NCHI NZIMA, LEO

Dodoma, leo
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye leo ameanza ziara ya kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, kabla ya kuanza ziara hiyo, Waziri Nape amesema tathmini inaonesha utekelezaji wa operesheni hiyo ni asilimia 69 huku baadhi ya maeneo yakiwa na changamoto na kutofanya vizuri akiitaja kwa mfano mikoa ya Tanga na Dar es Salaam.

“Kwa muda uliobaki tumekubaliana tuongeze nguvu kwa kutoka ofisini na kuifikia mikoa yote nchi nzima ili kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa operesheni ya Mfumo wa Anwani za Makazi unaojumuisha ukusanyaji wa taarifa, kuweka taarifa kwenye mfumo wa kidijitali na uwekaji wa namba za nyumba, majina ya barabara na mitaa”, Amezungumza Waziri Nape.

Ameongeza kuwa, Operesheni ya anwani za makazi inalenga kuhakikisha kila mtanzania anatambulika mahali alipo, mahali anapofanyia kazi/biashara na anapoishi hivyo ushirikiano wa pamoja utaifanya nchi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo unaweza kupata huduma ukiwa nyumbani kwako

“Katika mazingira haya ya dunia inayokwenda kidigitali si vema kwa nchi kuachwa nyuma, tumuunge mkono Mhe. Rais Samia kwenye operesheni hii na tujitendee haki watanzania kwa kuhakikisha tunakuwa na Anwani za Makazi”, amesisitiza Waziri huyo

 Aidha, katika ziara hiyo Waziri Nape ameambatana na Dk. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na baadhi ya wataalamu ambapo wanatumia usafiri wa helkopta ili kuifikia mikoa zaidi ya mitatu kwa siku, kwa kuwa zoezi hilo ni operesheni maalumu na Wizara imejipanga kwenda kuona mwenendo wa utekelezaji na kuongeza nguvu maeneo yenye Changamoto.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana