Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akimpa zawadi ya pesa Mtoto Kabula Mussa mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Makongolosi, Chunya Mkoani Mbeya baada ya kumuona akifanya biashara ya kuuza ndizi.
Akiwa katika mkutano na Wananchi wa Chunya, Dkt. Tulia alimuona mtoto huyo ambaye alikuwa akizunguka katika uwanja wa mkutano akifanya biashara yake ndipo alipoamua kumuita na kuwaeleza Wananchi kwamba.
“Nimevutika na mtoto huyu ambaye nimemuona hapa akiuza ndizi, niwaeleze tu kwamba mimi mwenyewe mwaka 1988 nilikuwa kama huyu binti na nilikuwa nikifanya biashara kama hii.
Kila mmoja wetu hapa ni kwamba kiukweli haijui kesho yake hivyo pia hatuwezi kujua huyu binti kesho atakuja kuwa nani hapa duniani hivyo tuwapende na kuwalinda” alisema Dkt. Tulia
Post a Comment