Waziri wa Madini, Dkt Dotto Biteko amewaomba watanzania kuwa watulivu hadi serikali itakapotoa taarifa za uhakika kuhusu Ruby inayodhaniwa inatoka Tanzania inayopigwa mnada Dubai.
Biteko aliyasema hayo alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu madini hayo yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 200 wakati wa semina ya Wabunge Wanawake, kuhusu fursa za uchimbaji madini iliyoandaliwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake katika Ukumbi wa Bunge wa Msekwa jijini Dodoma Aprili 23, 2022.Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Biteko akilitolea suala hilo ufafanuzi....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment