Jumatatu, tarehe 16.5.2022, KAMATI YA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO wa Jimbo la Musoma Vijijini kimefanya KIKAO cha kugawa fedha hizo.
Kikao kimefanyika kwenye Ofisi za Halmashauri yetu (Wilaya ya Musoma, Musoma DC) chini ya Mwenyekiti wake, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
UAMUZI
1. Vifaa vya ujenzi vinunuliwe na Halmashauri yetu na viwe tayari kugawiwa ifikapo Jumatatu ijayo, tarehe 23.5.2022
2. Fedha zilitolewa na Serikali ni Tsh 52.43 million na vifaa vitakavyonunuliwa ni:
Mabati 852 (bando 71)
Saruji Mifuko 596
Nondo 202
SEKONDARI ZILIZOTUMA MAOMBI NI:
1. Kigera 2. Kiriba
3. Mkirira 4. Seka
5. Nyakatende
6. Makojo
7. Nyasaungu (mpya, inajengwa)
8. Murangi 9. Tegeruka
10. Mugango 11. Bulinga
USAFIRISHAJI WA VIFAA VILIVYOGAWIWA
Sekondari iliyogawiwa vifaa vya ujenzi inalo jukumu la kusafirisha, kwa gharama zao, vifaa hivyo.
TAREHE YA MWISHO YA KUTUMIA VIFAA VILIVYOGAWIWA
Ifikapo tarehe 30.7.2022, vifaa vyote vilivyogawiwa lazima viwe vimetumika kama ilivyopangwa. Watakaoshindwa kufanya hivyo, vifaa hivyo vitaondolewa na kupelekwa kwenye Sekondari nyingine yenye mahitaji ya kuvitumia.
PICHA ya hapa zinaonesha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa na Washiriki wa Kikao cha kugawa Fedha za Mfuko wa Jimbo.
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
https://ift.tt/DvnNCju
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
https://ift.tt/DvnNCju
Post a Comment