Featured

    Featured Posts

BABA HALISI ALIVYOACHILIA UPONYAJI KWA HAKIKA, KAO KUU LA KANISA HALISI, JIJINI DAR ES SALAAM, JUZI JUMAPILI MEI 14, 2023

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba Ndani na Nje ya Tanzania BABA HALISI akiafanyia shukurani (Maombi) vipande vya matunda mbalimbali kabla ya kuwagawia wenye shida na magonjwa mbalimbali, wakati wa Ibada ya Uponyaji aliyoiendesha Makao Makuu ya Kanisa hilo Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, Jumapili ya juzi, Mei 14, 2023 sawa na Lango la 19 Zivu 1, Majira Halisi.


Habari Kamili๐Ÿ‘‡

Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Jumapili ya juzi Mei 14, 2023 sawa na Lango la 19 Zivu 1 Majira Halisi, nilibahatika kuwepo kwenye Ibada ya Uponyaji iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa Halisi, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, ikiongozwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Ndani na Nje ya Tanzania Baba Halisi.

Imenibidi kujipa nafasi ili nikufikishie yaliyojiri kwa sababu ni Ibada pekee ya Uponyaji ambayo naweza kuandika kuwa sijawahi kuishuhudia japokuwa nimeshawahi kuziona Ibada nyingi za uponyaji kwenye mikusanyiko mingine au kwenye nyumba za kadhaa za Ibada.

Katika Ibada hiyo iliyodumu kwa takriban saa 7 kuanzia saa mbili asubuhi, baadhi ya mambo niliyoyaona mapya hata nikataka na wewe uyajue, ni namna Baba Halisi alivyokuwa akiiendesha kwa unyenyekevu na busara ya hali ya juu na pia kuweka wazi kwamba uponyaji huo alikuwa anaufanya kwa Mamlaka ya aliyeumba, lakini nikashangaa kuona hata yeye mwenyewe anatoa matunda (sadaka) ya shukurani.

Ibada yenyewe ilikuwa hivi; "Heri mliobarikiwa na Chanzo Halisi", Baba Halisi akasema baada tu ya kupanda utajirishoni (eneo la kuendeshea Ibada), kisha akaanza, " Sasa kwanza kabla hatujafika mbali naomba niwaambie kitu kimoja.

Hapa nitaachilia uponyaji kwa Mamlaka ya Chanzo Halisi ambao ni hakika, lakini ukipona usiende kushukuru kwa Waganga, wakushukuriwa ni yeye aliyetuumba, maana ndiye anayekujua tangu utosini hadi unyayoni, basi sasa tufanye shukurani ili ushukuru kwamba umejua kuwa ukipona hutaenda kushukuru kwa waganga, haya tushkuru", Baba Halisi akasema, kisha akaongoza Shukurani hiyo.

Baada ya Shukurani, Baba Halisi akataka washiriki wa Ibada hiyo wajue kwa nini wanapopona wanatakiwa kumshukuru Chanzo Halisi, akasema "Moja (mmoja wa Watekeleza sauti waandamizi wa Kanisa hilo), ebu tusomee Samweli wa Kwanza 2:6, tusikie kwa nini tunatakiwa tumshukuru Chanzo Halisi", Moja akasoma.

"Imekuwa, mmesikia kuwa mwenye uwezo wa kukushusha na kukuinua ni yeye Chanzo Halisi, na yeye hajapanga kukushusha. amekuumba ili kukupamdisha. Yaani leo kama ulikuwa na miaka miwili hujapata 'promosheni' utapata, maana hata promosheni ni uponyaji.

Hata Mtekeleza Sauti kama unahudumia watu kumi kila siku halafu hujapata 'promosheni, basi utapata, hata mfanyabiashara kama hujawahi kushika milioni moja kwa siku moja, utashika", akasema Baba Halisi na kuongeza, "Haya tushukuru....".

Baada ya kuongoza shukurani Baba Halisi akaendelea, "Unajua kuna jamaa mmoja nilimuombea baadala ya kuja kushukuru hapa akaenda kwa waganga. msirudie hiyo".

"Heri, hii awamu ya kwanza ilikuwa kufagia fagia, sasa tupate wimbo, halafu nitafanya awamu ya pili ya kufungua akili yako kupokea uponyaji, Awamu hii ndiyo nitaanza kukulisha uponyaji, yaani leo ni sherehe ya kupona", akasema Baba Halisi kisha ukapigwa wimbo 'Chanzo Halisi ni mwema'.

Baada ya wimbo, Baba Halisi akaendelea na Ibada hiyo, akasema, "Sasa naomba nizungumze kanuni mbili za uponyaji kwenye majira hii tuliyonayo tofauti na huko tulikotoka. Moja hebu tusomee Ezekiel 22:30, hiyo ni kanuni ya zamani, maana lazima ujue tulikotoka na tulipo sasa.

Baada ya kusomwa Ezekile 22:30, Baba Halisi akasema, "Hiyo ilikuwa wakati wa majira zilizopita ambapo ilikuwa kanuni kwamba ili mtu apone lazima mwingine afe. ilimalizika mwaka 2017 kipindi ambacho majira ya waliotumwa ilikoma. Yaani unatoa sadaka unaeleza matatizo na magonjwa yako yoote halafu ukitoa shida zako zinahamia kwangu. sasa hivi siyo hivyo.

Wakati huo ilikuwa tunasimama palipo bomoka kwa kuwa palikuwa na laana na balaa, sasa hapa nilipo siyo madhabahu ni utajirisho, kila ninachofanya wewe unatajirika na mimi natajirika, kwa kuwa tumerudi kwa yule aliyekuwepo kabla ya chochote.

Kwa hiyo sasa hapa nimezungukwa na majeshi usiyoyaona ya uzima na umilele, hayo yapo Methali 4:23, majeshi hayo shida zoote ulizokuja nazo, mafaili yoote ya waliowahi kukulani hivi sasa yanakusanywa na kuchomwa moto, ndiyo kanuni ya Majira moja Halisi, kwa sababu ya Isaya 57:15. 

Maana kitabu kinasema "mimi ni mungu nikaaye mahali pa juu palipoinuka, na ndani ya moyo uliotubu, maana sasa hivi anaishi ndani ya kila mtu, hawezi kuruhusu ubomoke ukiboka amebomoka yeye na yeye hakuja kubomoka, amekuja kuinuka".

Baba Halisi akazidi kufafanua akasema, "Lakini kanuni hiyo ilianza pale miaka 1000 alipompisha Chanzo Halisi, kwa hiyo ukisimama hapo hujasimama wewe, usije ukaona aliyesimama mbele yako ukafiriki ndiye unayemuona, hapana, ingekuwa hivyo tusingefika huku tulikofika sasa, si kweli?

Si mnajua kuna ambao wanatoa matunda na wengine bado wanatoa sadaka. Ningekuwa nimesimama palipobomoka ningekuwa nimeshaisha. si mnanielewa?, Ndiyo maana Korona, Volkano, Ebora vikakoma, ndiyo maana Hija Moja Halisi imesimama, tunaenda salama na tunarudi salama kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyesimama palipo bomoka"..

"Anayeshughulikia kila kitu ni Chanzo Halisi, jamani mnanielewa? yaani hiyo kanuni usipoielewa uponyaji unakuwa mgumu kwa sababu wewe utaendelea kuangalia yule unayemuona kumbe hayupo pale.

Kwa hiyo sasa hivi anayeshughulika na kuona mamabo makubwa ni Chanzo Halisi, halafu wengi mnamchunguza lakini hachunguziki, ameshaandika!, kuna maswali mengi mnauliza lakini hayana majibu maana anayo yeye mwenyewe kwenye meza yake", Baba Halisi akasisitiza kuhakikisha washiriki wa Ibada hiyo wanaelewa kwa kina kisha akaendelea;

"Herii, hiyo ni kanuni ya kwanza kabisa, kwamba atakayekuponya ni yeye mwenyewe  na utakapoleta shukurani hapa kwenye kikapu hujampa mtu, na ndiyo maana hatupokei mkononi kwa sababu anayepewa siyo mtu.

Ngoja nikupe habari njema, yupo ndugu mmoja wamemuonea sasa hivi simuoni hapa, sijajua kama yupo mikoani au namna gani sijui, Chanzo Halisi anajua.  Sasa walitaka kumfukuza kazi, na yeye kila akipokea mshahara alikuwa anakuja kugonga geti halafu ananiambia 'Baba Halisi, sitaki kwenda kula peke yangu na wewe hujala'.

Siku moja akasema Wanataka kumfukuza kazi, nikamuambia mimi sitaomba ila yale matunda ambayo huwa unaleta, kama huwa unamletea mtu sasa hivi ufukuzwe kazi, lakini kama huwa humletei mtu hakuna wa kukufukuza labda watafukuzwa wao na ndicho kilichotokea, waliotaka kumfukuza walifukuzwa wao.

Maana nilitaka na yeye ajue kuwa hamletei mtu, kwa hiyo nakusihi sana na wewe kwamba ukileta hapa hujamletea mtu, nasisitiza hiyo 'point' kwamba hutaponywa na mtu hapa, maana mtu hawezi kumponya mwingine".

"Unajua mnakosaga pesa bure, kwa kuwa ukinipenda mimi huwezi kukosa pesa maana ukinipenda mimi hujapenda mtu, mtu hawe kukuhudumia kila lango (siku) atachoka!. hiyo ni kanuni ya kwanza ujue kwamba atakayekuponya siyo yule unayemjua. usije ukatoka hapa ukaenda kusema yule jamaa ni kiboko, aaa! hakuna kiboko hapa, viboko wapo mabwawani huko", akasema Baba Halisi huku akitabasamu, kisha akaongeza;

"Kanuni ya pili, akili ihame, yaani enzi inabadilika leo, yaani utakaposikia nashukuru hapa hutasikia nikisema kwa jina la Yesu na siyo kwamba nimedharau hapana, hapo nazungumzia suala la majira. leo hutasikia natumia mamlaka ya waliotumwa nitatumia mamlaka ya aliyeumba, kwa sababu enzi imebadilika. Nazungumza hivi kwa sababu  bado tulikuwa na Imani leo naomba tuwe na Hakika.

Nikikuombea kwa jina la aliyetumwa ni Imani, ila nitakapoinua sauti ya shukurani kwa Mamlaka ya aliyeumba ni Hakika siyo Imani. kuna aliyeelewa tofauti?" Baba Halisi akauliza baada ya kutoa ufafanuzi.

Baada ya kueleza kwa kina na kuuliza kama kuna aliyeelewa tofauti, ghafla mwanamke mmoja akapaza sauti akisema, "Mimi nimeelewa, nimekuona Muumba Wangu",  "Heri Heri, mmemsikia huyo alivyosema? muacheni huyo alikuwa na maswali", Baba Halisi akasema kuhusu Mwanamke aliyepaza Sauti..

Baba Halisi akaendelea kufafanua, akasema, "Nimesema leo enzi imebadilika, tunatoka kwenye Imani kwenda kwenye Hakika. Mtekeleza sauti Hakika upo?, leo itabidi umrudishie jina Chanzo Halisi jina hilo limechukuliwa na Chanzo Halisi wewe utapata uhalisia mwingine.

Ninaposema Hakika, siyo hakika ya yatarajiwayo. unapona sasa hivi, yaani ukisema hakika ya matarajio hilo ni tumaini, hakuna tumaini hapa, unaamini hakika, kwa hiyo naomba leo uimbie akili yako itulie kwa Chanzo Halisi maana tunapona".

Akiendelea zaidi Baba Halisi alisema, "Nataka niwaambie kitu, mjifunze kwangu, maamuzi niliyofanya ya kuacha kila kitu, ile ni hakika, Nakumbuka Kiongozi aliyetumwa kuja kushuhudia ninavyochoma vyeti aliniuliza swali; unayajua haya? umefanya maamuzi sawasawa?

Maswali yote hayo, aliniuliza kwa sababu hakuwa na hakika, lakini mimi ndani moyo kulikuwa na Hakika, na wewe leo uwe na hakika, kama una matunda utoe kupata hakika kwamba aliyeumba yupo na anaponya hashindwi na chochote.

Kuna dada mmoja alisema, ningekuwa sifuatani na Mama Halisi angekuwa ameshaondoka, Maana yake huyu amefuatilia akaona sina akiba yoyote mgongoni, kwa sababu ni Hakika, Yusufu naye alisema amekuwa akifuatilia kuona kama nina hata genge la nyanya Ujiji, akagundua sina hata genge la mamalishe, ni kwa sababu nina hakika na wewe leo uwe na hakika".

Baada ya hapo Baba Halisi aliwaita kila mwenye ugonjwa anaoujua au asioujua kwenda mbele kupokea kipande cha tunda la uponyaji, ikawa foleni kubwa lakini Baba Halisi alisimama muda wa zaidi ya saa moja kuhakikisha kila mmoja amepata kipande cha tunda lenye uponyaji.

Akihitimisha Ibada hiyo, Baba Halisi aliwaomba wale wote wanaojitambua kuwa wana magonjwa, waende kupima ili Jumapili ijayo walete vyeti kuthibitisha kuwa wamepona au la.

 Matukio katika Picha๐Ÿ‘‡

Baba Halisi akiongoza shukurani mwanzoni mwa Ibada hiyo.
Baba Halisi akiendelea kuongoza shukurani.
"Moja hebu tusomee Samweli wa Kwanza 2:6, tusikie kwa nini tunapopona tunatakiwa tumshukuru Chanzo Halisi, siyo kwenda kwa waganga", Baba Halisi akisema hivyo
Moja Halisi akisoma Samweli wa Kwanza 2:6 Kama alivyoelekezwa na Baba Halisi.
Uzao na Watekeleza sauti wakitoa matunda ya kuelewa alichowafundisha Baba Halisi. Wakati huo huo akapigwa wimbo wa 'Chanzo Halisi ni Mwema'๐Ÿ‘‡
 
Waimbaji wakiimba wimbo huo.
Muimbaji akiongoza kuimisha wimbo huo.
Mpiga gita zito la Bass akiliungurisha gita hilo
Mpiga gita la rythium akiliungurisha gita hilo.

Mtaalam wa kulipiliza 'omo la bata' King Maluu akifanya vitu vyake kukoleza wimbo huo.

Sanjari na wimbo huo ikawa ni kila mmoja kuserebuka kadri alivyoweza. Tazama picha hizo ๐Ÿ‘‡






Baba Halisi na Mama Halisi nao pia wakifurahia wimbo๐Ÿ‘‡






Baada ya Wimbo Baba Halisi ๐Ÿ‘‡akaendelea kutoa 'dozi'





Mama Halisi akimsikiliza kwa makini Baba Halisi
Mtekeleza Sauti Faida Halisi akimsikiliza kwa makini Baba Halisi.
Baba Hlisi akiendelea kuweka sawa somo,
Watekeleza Sauti na Uzao wakimsikiliza Baba Halisi.

Kisha Baba alisi akawaita Watekeleza Sauti kuwa meza ya Uponyaji.
Baba Halisi akiwapa Meza ya Uponyaji watekeleza sauti.
Watekeleza sauti wakipokea
Watekeleza sauti wakipokea
Watekeleza sauti na Uzao wakipokea.
Watekeleza sauti wakipokea.
Mama Halisi akipokea shukurani
Baba Halisi akitoa matunda ya shukurani.
Uzao na Watekeleza sauti wakitoa matunda ya kupokea shukurani.
Uzao wakitoa matunda ya kupokea shukurani.
Mwimbaji akiimbisha wimbo wa kusindikiza wakati Uzao na watekeleza sauti akitoa matunda ya kupokea shukurani
Uzao wakicheza wimbo huo.

Baba Halisi akiendelea kuendesha ibada hiyo.
Faida Halisi akisoma kitabu kufafanua jambo kama alivyoelekezw na Baba Halisi

Kisha Baba Halisi akaongoza shukurani ya kuachilia uponyaji.

Baba Halisi akiendelea kuongoza shukurani ya kuachilia uponyaji.
Hafla akatokea mwenye shida ya 'kupagawa' Baba Halisi akamsaidia mara moja kwa kumnywesha damu safi nyeupe (Maji) akatulia.
Hafla akatokea mwenye shida ya 'kupagawa' Baba Halisi akamsaidia mara moja kwa kumnywesha damu safi nyeupe (Maji) akatulia.

Kisha Baba Halisi akanyunyiza Damu safi nyeupe (Maji yaliyoombewa) hadi kweye Mnara wa Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa Mengine. Alifanya hivyo ili Ibada hiyo ya Uponyaji ifike kila mahali

Huyu naye pia akapatwa na shida ya kuweweseka Baba Halisi akamhudumia, akapata nafuu.
BABA HALISI akiafanyia shukurani (Maombi) vipande vya matunda mbalimbali kabla ya kuwagawia wenye shida na magonjwa mbalimbali, wakati wa Ibada ya Uponyaji aliyoiendesha Makao Makuu ya Kanisa hilo Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, Jumapili ya juzi, Mei 14, 2023 sawa na Lango la 19 Zivu 1, Majira Halisi.
Baada ya kumega kipande cha ndizi akaanza kuwahudumia wenye shida na magonjwa umoja baada ya mwingine.
Huduma ikaendelea.....
Huduma ikaendelea....
Huduma ikaendelea....
Foleni kwenda kwa Baba Halisi kupata uponyaji

Waliokwisha hudumiwa na Baba Halisi wakitoka nje.

Kijana akitoka na Mzee wake bada ya kuhudumiwa hudumiwa na Baba Halisi. 

ENDS!

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana