Featured

    Featured Posts

DC TUKAI ATAKA WAZAZI KUWALINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai akizungumza na wageni waalikwa hawapo pichani sikubya familia Duniani. Na Odace Rwimo, Nzega
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwalinda Watoto wao juu ukatili unaefanyika ndani familia na jamii kwa ujimla .

Wito huo ameutoa katika Maadhimisho ya siku ya familia Duniani iliyofanyika kiwilaya katika ukumbibwa halmshauri ya wilaya ya Nzega Mkoani hapa.

Alisema suala la malezi na makuzi no jukumu la Kila mzazi/mlezi katika kuangalia mwenendo wa mzima wa malezi ya mtoto tangu akiwa tumboni maana sayansi ya malezi ya awali ya mtoto inathibitisha kwamba malezi huanzia tumboni.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi Wa serikali na taasisi mbalimbali za Uma na vyama vya siasa siku ya Familia Duniani

Tukai alisema Kuna baadhi ya Mambo mhumu ya kuzingatia katika makuzi ya mtoto ambayo ni pamoja kutenga mda wa kukaa na familia yako,kutoa nasaha juu ya maadili mema,kutokutoa ahadi zisotekelezeka kwa mtoto,kutumia maneno makali ya kumkatisha tamaa mtoto.

" Wazazi na walezi kwa ujumla tumejikuta tukifanya ukatilii juu wa watoto wetu bila ya sisi wenyewe kujua mfano unajikuta ukutumia kauli za ubinafasi,manung'uniko kuhusiana na gharama unazotumia juu yake sanajari na ukosoaji usiokuwa na maadili kwa mtoto juu ya muonekano wake wa nje pia na huo ni ukatili" alisema Tukai

Aidha Kuna umuhimu mkubwa sisi Kama wazazi kukumbushana juu ya malezi ya watoto wetu kwani kwa Sasa Kuna kuporomoka kwa maadili katika jamii zetu Hali ambayo inachangia kuongezeka kwa ukatilii wa kijinsia na unyanyasiji kwa watoto wetu.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Halmshauri ya wilaya ya Nzega Mariam Masinde alisema inapaswa Sasa kuendani na kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya familia Duniani " kuwa na familia Bora inawezakana ,malezi Bora ni Chachi ya Ustawi wa Jamii na Taifa kwa ujumla tukishirikiana katika kutokomeza ukatili wa Kijinsia".

Alisema Kuna umuhimu mkubwa kuieleza Jamii juu ya masuala ya ukatili wa Kijinsia na ukatilii dhidi ya watoto ambayo ni Hali ya kutumia nguvu na Mara nyingi hutokea madahara kwa mtu anayefanyiwa ukatili.

Afisa Ustawi wa Jamii Halmshauri ya Mji Nzega Mariam Masinde akitoa Elimu namna Bora ya kukabiliana na ukatilii wa kijinsia katika jamii zetu.

Alisema Kuna viashiria vingi mfano migogoro ya Mara kwa mara,Mazingira yasiyorafiki na dalili za mtu aliyefaniwa ukatilii aidha kwa mtoto huanza kuwa muoga ama kujitenga tofauti na kawaida yake,jusikia vibaya na wakati mwingine kupoteza Nuru ya uso wake.

Masinde alisema kufauatia dalili hizo Kama mzazi ama mlezi ni vyema kufuatlia mienendo ya mtoto wako ili kujua anapitia wakati gani na kitungani kimempata ili uweze kuchukuwa hatua za kuweza kunisaidia muasirika wa ukatili wa Kijinsia.

 Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya Mji Nzega Wambura Mkono awali katika Risala yake kwa mgeni rasimi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Nzega  Naitapwaki Tukai alisema wilaya ya Nzega inakusudia kujenga Jamii yenye maadili na kuhushimiana ilinkuweza kuepuka ukatili wa Kijinsia.

Alisema tunahitaji kujenga familia zenye wazazi wote wawili wenye mwelekeo mmoja nanmaelewano ya kutosha ,kwanindio msingi wa uzalishaji Mali utakowawezesha kutoa hufuma za msingi kwa watoto wao na kufuatilia Karibu makuzi na malezi ya watoto.

Alisema ili kuwa na familia zenye maadili na upendo ,Serikali inapendekeza
Wanafamilia baba,mama,watoto,ndugu wa Karibu kukaa pamoja ili kujadili mafanikio katika familia na kupongezana lakini kujadili changamoto zilizopo ili kuitafta majawabu ya pamoja kwa amani na upendo .
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana