Featured

    Featured Posts

DC KYERWA APIGA MARUFUKU WATOTO KUFUNGIWA CHAKULA KIPORO (PAMBA) SHULENI.

Na Lydia Lugakila, Kyerwa.


Mkuu wa Wilaya ya  Kyerwa Mkoani Kagera, Zaitun Msofe amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Wazazi, kuwapa Watoto Chakula kiporo maarufu Pamba ili waende nacho na wakitumie shuleni.


Msofe ametoa kauli hiyo kupitia kikao Cha baraza la madiwani kilichofanyika Wilayani humo alipopata nafasi kutoa  maelekezo ya Serikali.


Amesema ni wakati sasa kupiga vita kwa hali na mali tabia hiyo kwani wapo wataalam wamepita na kuona kwamba mtoto anachukua kiporo cha Chakula kilichopikwa tangu Jana usiku ambacho mtoto ukitunza na kwenda nacho shuleni.


"Mtoto anashinda na Chakula kuanzia asubuhi hadi mchana anapoenda kukila kinatoa povu kimeishaharibika ebu tuwahudumie watoto tuseme Pamba basi" alisema Mkuu huyo wa Wilaya.


Amesema ni wakati Sasa wa wazazi kufuata mwongozo wa Serikali wa kuwachangia chakula shuleni ili watoto wao wapate lishe Bora.


Ameongeza kuwa lishe katika Wilaya ya Kyerwa haiko vizuri kwani Wananchi wamezoea kutumia chakula kimoja ambacho ni ndizi.


Amewasisitiza Madiwani hao kuhakikisha wanaendelea kutoa Elimu kwa Wananchi ili wazingatie mlo kamili wasitumie ndizi  tu kama chakula peke yake.


Aidha amelipongeza Baraza la Halmashauri hiyo kutokana na ushirikiano mzuri ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bahati Henerco kwa niaba ya madiwani hao ameahidi kuyatekeleza vyema maelekezo ya Serikali huku akimpongeza Rais Dokta Samia kwa kuendelee kuijenga Kyerwa katika sekta mbali mbali ikiwemo ya afya Elimu.


Hata hivyo amewaomba madiwani hao kuweka jitihada zaidi kudhibiti Magendo ya Kahawa.

Sehemu ya Madiwani wa Halmashauri hiyo pamoja na Viongozi mbali mbali.


Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaitun Msofe akizungumza katika kikao Cha baraza la madiwani.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana