Featured

    Featured Posts

MWAJABU MBWAMBO ASISITIZA SERIKALI YA RAIS SAMIA INAPASWA KUPONGEZWA KWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI MIJINI NA VIJIJINI NDANI YA MIAKA MIWILI TU

Dar es Salaam
Mwenyekiti Umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo amesisitiza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, inapaswa kupongezwa kwa kufanya mambo makubwa ndani ya miaka miwili tu.

Amesema, chini ya Uongozi wa Dk. Samia Serikali imeweza kufanikisha miradi 1373 ya Maji kwa vijiji 2649 na kufanikisha jumla ya vijiji vyenye maji kufikia 9737 nchini, na kwa upande wa mijini miradi ya kusambaza maji 80 imekamilika huku miradi mingine mingi ambayo imegharamiwa na mfuko wa maji wa Taifa ikiendelea kutekelezwa.

Mwenyekiti Mbwambo amesema hayo wakati akitoa mada kuhusu 'Miradi ya Maji Tanzania Fursa Kwa Vijana' katika Kongamano la Umoja wa  Vijana wa CCM (UVCCM) Seneti ya Vyuo na vyuo Vikuu lililoandaliwa na Seneti Tawi la Abiyan Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Walengwa wakiwa vijana kutoka Seneti ya vyuo 36 mkoani Dar es salaam.

Kongamano hilo limefanyika katika Hotel ya Land Mark Dar es salaam, kujadili Mada inayosema Ushiriki wa Vijana katika Siasa na Uchumi"

Mwenyekiti Mwajabu aliwajuza vijana kwamba kukamilika kwa miradi hii ni fursa kwa vijana kuweza kujiajiri katika kilimo, ufugaji, kuanzisha biashara ya maduka ya vifaa vya maji kwani itahitaji kukarabatiwa, vijana kupata fursa ya kuongeza ujuzi kwenye eneo linalohusiana na mirad ya maji.

Aliwafunda vijana kuhakikisha wanaongeza ujuzi katika vyuo vya kati ili kuwa wabobezi na weledi na kujikita katila fursa zilizozalishwa na miradi ya maji. Kwani Dr Samia Rais wa JMT ametekeleza ilani kwa vitendo ni jukumu la vijana kuchangamkia fursa.

Pia amewasa  vijana kujifunza kubana matumizi na kuweka akiba, kuacha starehe, anasa na kujikita na kudumu katika eneo moja ili kubobea zaidi na kuwa mahiri katika eneo hilo pale wanapoamua kujiajiri. Kwani. Kwani vijana wengi hawana ujuzi hivyo ni lazima  kujikita zaidi kuongeza ujuzi.

Mwenyekiti Mwajabu Mbwambo alikuwa miongoni mwa watoa mada walioshiriki. Watoa mada wengine ni Mhadhiri kutoka Udsm Dr Kahangwa, Mhadhiri kutoka IFM Madam Siriel Nchembe, Mbaraza UVCCM kutoka Ubungo Komredi Dorcas.
Mwenyekiti Umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akitoa Mada katika Kongamano Maalum la UVCCM, lilofanyika Hotel ya Land Mark jijini Dar es Salaam, jana.
Mwenyekiti Umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo akiendelea kutoa Mada katika Kongamano Malum la UVCCM, lilofanyika Hotel ya Land Mark jijini Dar es Salaam, jana
Washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Mwenyekiti Mwajabu wakati akitoa Mada.
Mwenyekiti Mwajabu akiwa pamoja na baadhi ya Viongozi wa UVCCM wakati wa Kongamano hilo.
Mwenyekiti Mwajabu akijadili jambo nje ya ukumbi na mmoja a Viongozi wa UVCCM.
Mwenyekiti Mwajabu akisindikizwa na baadhi ya Viongozi wa UVCCM alipokuwa akiwasili kwenye Kongamano hilo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana