Featured

    Featured Posts

MTEMVU AWASIFU WENYEVITI WA MITAA WANAWAKE DAR ES SALAAM, ASEMA NI WAAMINIFU KAMA RAIS SAMIA, AWATAKA WANAUME KUWAIGA.

Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtevu amewasifu Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wanawake mkoa huo akisema ni waaminifu kama Rais Samia Suluhu Hassan, na kuwataka Wenyeviti Wanaume wasio waaminifu kubadilika na kuwaiga wanawake hao.

Sanjari na kauli hiyo, Mwenyekiti Mtevu ameonya kuwa Watendaji wa Mitaa hasa Wanaume ambao siyo waaminifu wasipobadilika sasa, watakapoomba kushika nafasi hizo tena katika Uchagzi ujao, hata majina yao yakipitishwa kwenye mitaa yao atayanyofoa.

Mwenyekiti Mtemvu aliyasema hayo, katika sherehe ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Msigani Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, kuwakabidhi kadi Wanachama wapya 400 wa Umoja huo, iliyofanyika jana.

"Wenyeviti wa Mitaa Wanaume wengi wao siyo waaminifu, wamekuwa wakisababisha vigogoro kadhaa ya ardhi, sasa kama wanahitaji kugombea tena nafasi hizo, wabadilike, maana watakapoomba hata kama wakipita katika mitaa wakoomba majina yao nitayanyofoa", akasema Mwenyekiti Mtemvu.

Mtemvu alisema, maeneo yenye migogoro na ubadhirifu wa aina mbalimbali ni yale yenye Wenyeviti wa mitaa wanawaume lakini mitaa ambayo Wenyeviti ni Wanawake hakuna migogoro na kama ipo ni michache sana kwa sababu Wanawake ni Waaminifu tena Wachapakazi kama Rais Samia.

"Mitaa yenye migogoro ya ardhi na ubadhirifu wa aina mbaimbali ni ile yenye Wenyeviti Wanaume, ile yenye Wanawake imetulia, hii ni kwa sababu Wanawake ni Waaminifu Kama Mwenyekiti wetu wa CCM Rais Samia ambaye kutokana na Uadilifu na uchapakazi wake Chama kipo Imara na Serikali anayoingoza imepiga hatua kubwa kimaendeleo katika nyanja zote", akasema Mwenyekiti Mtemvu.

Katika hafla hiyo ambayo iliandaliwa na Kamati ya Utendaji chini ya Mwenyekiti wa UWT Kata hiyo ya Msigani Winifrida Muhinja, Mwenyekiti Mtemvu aliahidi kutoa msaada wa Cherehani tatu kwa ajili ya Mradi wa Ushonaji wa Kinamama wa UWT Msigani.

Mbali na kuchangia Cherehani hizo, pia aliendesha harambee ya kukusanya fedha kwa kunadi keki ambayo kila aliyetaka kulishwa alichangia kiasi cha fedha kwa ajili ya Mradi huo wa Ushonaji, ambapo viongozi na watu mbalimbali walijitokeza.

Aidha Mwenyekiti Mtemvu katika hotuba yake, aliwataka Wana CCM na Jumuiya zake zote kuwa kitu kimoja ili kuimarisha mshikamano ambao ndio utakuwa chachu ya kuwezesha CCM kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akizungumza katika Hafla ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Msigani Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, kuwakabidhi kadi Wanachama wapya 400 wa Umoja huo, jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Kata hiyo Winifrida Muhinja na Kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia mkoa mkoa huo Juma Simba Gadaffi.

MFULULIZO WA MATUKIO KATIKA HAFLA HIYO

Mwenyekiti Mtemvu akiwasili ukumbini.
Wanachama UWT wakishangilia wakati Mwenyekiti Mtemvu akiingia ukumbini.
Muumini wa Kikristu akiomba Mungu Hafla ifanyike kwa amani na utulivu.
Muumini wa Kiislam akimuomba Mungu Hafla ifanyike kwa amani.
Wenye shughuli na waalikwa wakiwa ukumbini.
Baadhi ya Viongozi waalikwa wakiwa ukumbini.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Malamba Mawili wakiwa ukumbini kusubiri kupewa Kadi za UWT
Kimama wakishangilia jambo ukumbini.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu UWT Wilaya ya Ubungo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kibo  Sophia Fitina akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Ubungo Mzee Mbowe akizungumza kwenye Hafla hiyo.
Mwenyekiti wa UWT Msigani Winifrida Muhinja akimkabidhi zawadi ya Picha Mwenyekiti Mtemvu
Mwenyekiti wa UWT Msigani Winifrida Muhinja akimkabidhi zawadi ya kitenge Mwenyekiti Mtemvu.
Mwenyekiti Mtemvu akiwa katika picha ya kumbukumbu na Viongozi wa UWT Msigani. Mwenye shati la Kijani ni M-NEC Gadaffi.
Mwenyekiti wa UWT Msigani Winifrida akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti Mtemvu akikabidhi Kadi ya UWT kwa Mwanachama mpya kutoka shule ya sekondari Malamba Mawili.
Mwenyekiti Mtemvu akikabidhi Kadi ya UWT kwa Mwanachama mpya.
Wanachama wapya wakila kiapo baada ya kukabidhiwa Kadi za UWT
Mwenyekiti Mtemvu, M-NEC Gadaffi na Mwenyekiti Winifrida wakishiriki kula kiapo
Mwenyekiti Mtemvu akikabidhi cheti cha Hongera kwa Mwenyekiti wa UWT Malamba Mawili Chausiku Warioba. Viongozi mbalimbali walikabidhiwa vyeti hivyo.
Diwani Msigani akikabidhiwa Cheti
Mwenyekiti wa UWT Ubungo Amina Mashauri akizungumza katika hafla hiyo
M-NEC Juma Gadaffi akizungumza na kumkaribisha Mwenyekiti Mtemvu kuhutubia
Mwenyekiti Mtemvu akishiriki kuimba wimbo wa kumsifu Rais Samia, katika Shamrashamra zilizoibuka kabla ya kuhutubia.
Mwenyekiti Mtemvu akihutubia
Wanachama UWT wakimshangilia Mwenyekiti Mtemvu.
Wanachama UWT wakimshangilia Mwenyekiti Mtemvu.
Mwenyekiti Mtemvu akikata Keki ambayo kisha ilinadiwa ili kupatikana pesa kutunisha mfuko wa mradi wa UWT Msigani.
"Haya njooni niwalishe hii keki, lakini kabla sijakulisha unatangaza utachangia shilingi ngapi kutunisha mradi wa ushonaji wa UWT hapa Msigani", akisema Mwenyekiti Mtemvu
Akamlisha Mwenyekiti UWT Ubungo.
Akamlisha pia Mwenyekiti UWT Msigani.
"Hongera Mwenyekiti Shughuli imefana", Mwenyekiti Mtemvu akimwambia Mwenyekiti UWT msigani Winifrida mwishoni mwa shughuli.
Mweneyekiti Mtemvu akiaga baadhi a wanachama wakati akiondoka.
Mweneyekiti Winifrida akimsindikiza Mwenyekiti Mtemvu wakati akiondoka baada ya ahafla.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana