Featured

    Featured Posts

MWAJABU MBWAMBO AWAFUNDA KINAMAMA KULINDA WATOTO, APONGEZA RAIS SAMIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KATA YA PUGU

Mei 12, 2023.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Rajabu Mbwambo leo amewapiga msasa kwa kuwapa semina kuhusu mbinu za kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto viongozi wote katika Kata ya Pugu, wilayani Ilala.

Ametoa semina hiyo katika hafla ya Maadhimisho ya kuelekea kilele cha siku ya Mama Duniani, iliyowakutanisha Viongozi wa matawi, Kata, diwani na Afisa Maendeleo ya Jamii Tawi la UWT Kisumu, katika  Kata hiyo ya Pugu waliohudhuria katika maadhimisho hayo, akiwa mgeni rasmi.

Katika semina hiyo Mwenyekiti Mwajabu aliwahimiza kinamama kuwa mstari wa mbele kulinda watoto na kutoa taarifa katika Mamlaka husika wakiona viashiria vya ukatili wa aina yoyote.

Pia amewakumbusha viongozi kujiandaa, kuwashawishi na kuwajengea uwezo Wanawake na Mabinti wenye sifa ili muda ukifika wagombee nafasi za uongozi ikiwemo nafasi za kuwa Wenyeviti wa Serikali za mitaa 2024.

Mwenyekiti Mwajabu amepongeza juhudi za Raisi Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha miundombinu ya elimu katika Kata ya Pugu kwa kujenga shule, kuongeza madarasa, matundu ya vyoo na ujenzi wa kituo cha Afya.

Katika Maadhimisho hayo Mwenyekiti pia aliwakumbusha wanawake kama kauli mbiu yao inavyosema Mama Imara kwa ustawi familia, kuhakikisha pamoja na majukumu waliyonayo jukumu la kwanza ni ustawi wa familia na malezi ya familia ili kuwa na kizazi chenye maadili mema.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Rajabu Mbwambo akitoa Semina katika hafla hiyo, leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Rajabu Mbwambo akiendelea kutoa semina katika hafla hiyo..
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Rajabu Mbwambo (Mwenye mtandio wa Bluu), akisindikizwa na Viongozi alipowasili kwenye hafla hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Rajabu Mbwambo, akikagua bidhaa zilizokuwa zikionyshwa na Mwanamama Mjasiriamali, wakati wa hafla hiyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana