Featured

    Featured Posts

BABA HALISI AWAFUNDA UZAO (WAUMINI) WAKE KUHUSU TOFAUTI YA 'MUNGU' NA 'CHANZO HALISI', NI WAKATI AKITOA SOMO LA KUFUMBUA 'FUMBO LA IMANI', KATIKA IBADA YA JANA JUMAPILI

Tegeta, Dar es Salaam
Kwa vyovyote iwavyo kila binadamu mwenye akili timamu anapaswa aamini kuwa ameumbwa na kama ameumbwa lazima awepo aliyemuumba maana hata vifaa tunavyotumia kama simu na magari visingekuwepo kama binadamu asingevitengeneza, na kwa kuamini hivyo ndiyo maana tunachokiona huwa tunauliza kimetenezwa na nani.

Basi ikiwa huwa tunauliza simu fulani au gari ya aina fulani imetengenezwa na nani na tukafuatilia hadi kumjua, ni kwa nini basi binadamu hatusumbuki kujua nani hasa aliyetuumba, baala yake tunahangaika hadi inafikia kuabudu ambavyo havihusiki katumba kwa kuwa na vyenyewe vimeumbwa!

Bila shaka kuna hila ziliozuka miongoni mwa binadamu wenyewe, ambao baada ya kuona watu wanajaribu kumtafuta aliyewaumba wao wakaziteka akili za wenzao hadi kufikia hatua ya kuwaaminisha kwamba vitu au watu wengine ndiyo wenye nguvu juu ya uhai wao.

Kutokana na sababu hiyo, hadi leo wapo binadamu wanaoabudu wanadamu wenzao, Wanyama, milima, majabali, na kama haitoshi wengine wamechonga sanamu na kuziabudu kuwa ndiyo Mungu hadi kufikia hatua ya kuwepo maelfu ya Mungu duniani.

Japokuwa wapo ambao bado wanaamini hadi leo kwamba yupo aliyewamba na ni Mungu, tatizo linalojitokeza ni kwamba, sasa ukimuomba au kumuabudu Mungu kwa kuita Mungu, inakuwa haijulikani huyo unayemuita Mungu ni yule mwenyewe aliyekuumba au ni hiyo Miungu wanadamu, Miungu Milima, Mingu Mizimu, au Mungu yupi?

Juzi Jumapili, nilibahatika kuwepo katika Ibada Moja iliyofanyika kwenye Kanisa linaloitwa Kanisa Halisi la Mungu Baba ambalo Makao yake Makuu yapo Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam.

Japokuwa nilikuwepo kikazi, lakini somo lililokuwa linatolewa na Safu Mkuu wa Kanisa hilo anayejulikana kwa jina la Baba Halisi, lilivuta masikio nkaamua kufanyakazi yangu huku nikisikiliza kwa makini somo hilo, maana liligusa pale nilipokuwa najiuliza kwamba huyu Mungu ambaye huwa namuomba na kumuabudu ndiye yeye hasa au?

Katika somo hilo ambalo Baba Halisi alisema ni 'Kufumbua fumbo la Imani', Baba Halisi alikuwa akieleza kwa kina kwamba kama unajua kuwa uliumbwa na yupo aliyekuumba basi lipo jina lake sahihi la kumtaja ili usije kujikuta unayemuomba ni Mungu Mnyama, Mungu Mtu, Mungu jabali maana wote hao wanaitwa Mungu!

Sasa kwa kuwa nilimeleza kuwa nilimsikiliza vizuri, japokuwa nilikuwa bize, lakini mengi ya msingi niliyashika vizuri, kwa hiyo nitatiririka kukuandikia hapa hatua kwa hatua Baba Halisi aliyofundisha, ili pengine na wewe utawe kuambulia la maana kama nilivyoambulia mimi....

" Heri Heri Mliobarikiwa na Chanzo Halisi", Baba Halisi alianza kwa salamu hiyo kuwasalimia wamini wake ambao katika Kanisa Halisi wanaitwa Uzao, kisha akasema, "Wengi wamekuwa wakitetereka kwa sababu ya fumbo".

"Kwa mwenyeji na kwa mgeni naomba unisikilize kwa upendo, nazungumza haya yote kwa upendo, sijamlenga yeyote, wala sijalenga dini yoyote, wala dhehebu lolote wala mtumishi yeyote, ila tu mimi nimelenga kufumbua fumbo ambalo sote tulizaliwa tunalikuta ila Chanzo Halisi amekuja kulifunbua mwenyewe.

Kwa hiyo ninayo mambo matano ambayo  nataka kuyazungumzia na si kwamba huyajui, unayajua, lakini leo nataka niyanyooshe ili na wewe umkamsaidie ndugu yako", akasema Baba Halisi, kisha akaendelea;

"Wengi wanapenda zaidi tukisema Mungu au Yesu, wanasikia raha, lakini ukisema Mungu au Yesu bado ni fumbo, maana kuna Miungu wengi na kuna Yesu wengi, ila leo nataka tuondoke tukijua yupo yule wa kweli aliyeumba ili tumuabudu huyo ambaye mafanikio yako kwake, ukombozi upo kwake, uponyaji upo kwake. Kwa hiyo hilo ni la kwanza ambalo nitaliongelea.

Jambo la pili ambalo nitaongelea ni viapo ambavyo tumeapishwa vikatutisha tukaogopa kumfuata aliyeumba. Maana mwingine anasema "hiki nilichokuambia ukisema tu utakufa". kwa hiyo mtu anaogopa kumbe hajui tu kwamba viapo vipo vya aina nyingi kama hicho tu alichoapishwa cha kumtisha hilo nitaliongelea kwamba nalo huwa ni fumbo."

Akiendelea, Baba Halisi alise "La tatu, ni kuhusu nani atakayehukumu, hilo nalo ni fumbo, wengi wanajua atakayekuja kuhukumu ni Yesu, lakini hilo ni fumbo la dunia, leo tunalifumbua, na wengi wametishika kweli mpaka wakarudi nyuma, lakini leo watarejea kwa Chanzo Halisi.

Fumbo lingine ni lile la Yohana 14:6 linalosema "mimi ni kweli, njia na uzima", kwa hiyo wengi wamekwama hapo, hawajui kwamba tumeshafika kwenye barabara, bado wako njiani, kwa hiyo hilo fumbo leo linafumbuliwa, maana limevuta wengi kweli, na hapa wananisikia kwa upendo kabisa".

"Heri. Fumbo la tano ni kukumbuka upendo wa zamani, sasa leo nataka tujue upendo maana yake nini na kwa nini hapa (kanisa Halisi) tunasema upendo ulipitiliza maana yake nini,Baba Halisi akaseme, kisaha akaongeza. "Heri, mpo na mimi?" Baba Halisi akauliza, Uzao wakajibu "Imekuwa".

"Leo mafumbo lazima yaondoke, kila kitu kitakuwa wazi leo, maana wengine mshaogopa mnamani kupitia madirishani, lakini naomba mkae vizuri kabisa muwe na amani, mimi siyo mtukanaji jamani msiogope. Naomba kila mmoja aniangalie ahakikishea ananiona kabisa ili uhakikishea unanielewa kabisa", Baba Halisi akasema.

Akianza kufafanua kuhusu Mungu anapaswa kuitwa jina gani, Baba Halisi alisema; "Heri, ukisema jina 'Mungu' peke yake, kuna watu wengine ni Mungu, Kuna vitu vingine ni Mungu, kuna mizimu mingine ni Mungu, kuna mapepo mengine ni Mungu, kwa hiyo ukisema Mungu peke yake tuambie unamaanisha yupi? na ukisema Yesu peke yake haitoshi, maana hata Mussa alikuwa Yesu, hata Eliya Mtishibi alikuwa Yesu, kila aliyetumwa alikuwa Yesu Maana yake Mwana.

Heri.  Kwa hiyo naomba leo mnisikilize kwa upendo kabisa kwamba ukisema Mungu peke yake, kila ukoo una Mungu wake, kila Lugha ina Mungu wake, kila kabila lina Mungu, kila  jamaa ina Mungu wake, kwa hiyo leo nataka tuongelee aliyekuwepo kabla ya chochote huyo ndiyo tumuabudu. kama unasikia moyo unaenda mbio uambie utulie usiogope maana leo lazima tuseme kweli ili wanaopona wapone.

Heri Heri, kwa nini hapa tunasema Chanzo Halisi, maana yake aliyekuwepo kabla ya nafsi, roho na mwili, maana katika Kutoka 7:1 watu walimuabudu Mussa na walimuita Mungu na iliandikwa ni Mungu lakini hakuumba, Ukisoma Yoshua 4:14 watu walimuabudu Yoshua mwenyewe wakamcha na imeandikwa walimcha lakini hakuumba alikuwa ni mtu, ukisoma Samweli wa kwanza 5 1:15 watu walimuabudu Dragon na kuna wengine hadi leo wanamuabudu Dragon lakini hajaumba, Sasa ukisema Mungu unamaanisha nini? sisi tukisema Chanzo Halisi tunamaanisha aliyeumba kila kitu.

Eliya Mtishibi alisema kama Mungu ila hajaumba, na alipotea wakamuona tayari huyo, sawa, lakini hajaumba, Mussa mpaka leo hakuna anayejua kaburi lake liko wapi lakini hajaumba. Leo tuelewane jamani, hilo fumbo leo liondoke, hata Matendo 19: 23-30 Atemi Mkuu anaabudiwa na walimwengu wote lakini hajaumba, mapaka leo ukienda Ugiriki utakuta sanamu zake barabarani, imeandikwa hadi kwenye kitabu kitabu anaabudiwa hadi leo, lakini hajaumba hata mjusi, kwa hiyo nikisema Chanzo Halisi jamani niko sawa. acheni kudanganywa

Ukisoma ufunuo 12:1 kuna Ishara ya kwanza huyo ndiyo ameabudiwa na wengi mno lakini hajaumba hata sisimizi, anaitwa Ishara ya kwanza Mbinguni hajaumba, Ukisoma ufunuo 12-3:4 kuna Joka wa zamani hajaumba, huyo ndiyo hila.

Heri, Jamani sawa. Ukisoma Jeremia 44:18 kuna Malikia wa Mbinguni hadi leo anaabudiwa na kuimbiwa nyimbo lakini hajaumba. Waliotumwa wote walikuwa ni Mungu kwa mujibu wa Yohana 1: 1-5 lakini hawajaumba. Kwa hiyo nikisema Chanzo Halisi niko sawa sawa, mbona mnatetereka, ila wewe ukisema Mungu inabidi utuambie ni yupi maana wapo wengi.

Siku moja mwaka 95 nilikuwa shinyanga na Watu fulani kuna ajali ya ndege ilitokea milima ya uruguru, wakasema lete fimbo tugige ubao, wakapiga ubao nikauliza ndiyo mnafanya nini wakasema tunaongea na Mungu wetu tukirudi tusipate ajali, nikauliza Ubao ndiyo Mungu wenu. Hiyo sijasoma kwenye kitabu nilikuwepo mwenyewe.

Heri, jamani mnanisikia nachoongea leo? Warumi 11:36 inasema yupo aliyekuwepo ambaye kila kitu kilitoka kwake na kila kitu lazima kirudi kwake, sasa huyo anayeondoka hapa anakupigia simu kwamba hapa hakuna Mungu anamaanisha Mungu yupi? ila sote tulizaliwa tunakuta fumbo hiyo sikulaumu, ila naomba ukishafundishwa usikubali tena kufuatana na fumbo. na mimi nilishasema kama hapa ingekuwa anayeabudiwa siyo Mungu wa kweli ningekuwa nimeshaondoka, niliposema sikuwa natania.

Unamtaka Mungu wa Ukoo au wa Kabila, au unamtaka yule aliyeumba umeshampata. Maana Yeremia 10:11 imeandikwa yule Mungu wa ukoo , wa kabila ataangamia maana hajaumba. sasa kwa nini mnadanganywa, na msiseme nimewahukumu jamani, leo fumbo lifumbuliwe".

Baada ya maelezo hayo baadhi ya uzao wakaanza kuweweseka, Baba Halisi akawasaidia huku akisema.
"Hiyo ni miungu ya Ukoo. inangamia".

Baada ya kueleza jina analotakiwa kuitwa Muumba, Baba Halisi aliwaomba Uzao (Waumini wake) sasa wasidanganywe na yeyote, akisema "Sitaki kusikia nimepigiwa simu eti hapa hakuna mungu, maana hata wewe una akili, wewe unaweza kudanganya watu hawa."

Kisha Baba halisi aliwataka waumini kusimama ili kufanya toba, kwamba Chanzo Halisi awasamehe na kwamba wajitetei kwa chochote waliliamini miungu isiyo ya kweli, maana walienda kutambika tukidhani ni mungu wa kweli.

Kuhusu Kiapo Baba Halisi alisema mtu hana haja ya kuogopa kiapo kwa kuwa kiapo ni roho, ni nafsi, siyo Moyo, akasema :Na ukitaka kujua kwamba kiapo siyo moyo mdiyo maana sijawahi kuwaapisha. sina sababu ya kukuapisha kwa sababu sijihami kwa chochote, nina uhakika na ninachokufundisha, Wewe unatakiwa unisikilize kile ninachokufundishan halafu utaamua kwa akili yako kama ni kweli au uongo".

Alisema, hakuna sababu ya kuogopa kiapo chochote kwa sababu iapo katika kitabu cha Hesabu 30 kuanzia mstari wa pili hadi wa kumi kimandikwa kuwa Binti akiwa kwa Baba kama hajaolewa kiapo chochote atakachoapa au kuapishwa Baba yake anakitengua, na aliyekwihaolewa kiapo chochote alichoapishwa kichwa (mume) wake anakitengua. na kufafanua kuwa mwiko wa kabila pia ni kiapo lakini level iliypo sasa ni ya moyo.

Mnateseka bure mkombozi alishakuja ndani ya nchi yupo moyon mwako. waambieni wenye visukari na kansa waje hapa wapone bure. mfano yule mzee wa tunduru alija hapa dakika tatu akapona.

Pia Baba Halisi alisema, kuhusu kwamba Yesu atakuja kuhukumu, siyo kweli. "Wengi wanasumbuka kwamba atakayekuja kuhukumu ni Yesu siyo kweli, imeandikwa Yohana 5: 19-23 kwamba baba hahukumu bali mwana, lakini baada ya Yesu kuwambwa  msalabani alinyang'anywa kila kitu pamoja na hukumu, sasa aliyebaki na hukumu ni Chanzo Halisi", akasema Baba Halisi.

















































author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana