Featured

    Featured Posts

BALOZI POLEPOLE AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA CUBA

Balozi na Mkuu wa Kituo cha Uwakilishi Mjini Havana, nchini Cuba Humphrey Polepole jana aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel Bermúdez


Baada ya kuwasilisha hati Balozi Polepole alifanya mazungumzo na Rais huyo wa Cuba na pamoja na mambo mengine alimpa salamu za mshikamano kutoka kwa Samia Suluhu Hassan.


Naye, naye Rais Díaz-Canel alimhakikishia ushirikiano mkubwa ambao umejengwa katika misingi imara na waasisi wa mataifa ya Tanzania na Cuba Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Kiongozi wa Mapinduzi ya Cuba Kamanda Fidel Castro. 


Wakati uo huo Balozi Polepole alikutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Elimu ya Cuba ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya siku ya Kimataifa ya Kiswahili itakayoadhimishwa  Julai 7, 2023.



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana