Featured

    Featured Posts

ILIKUWA PATASHIKA BONANZA LA CHUO CHA MIPANGO, MBOGWE+video

Imekuwa patashika nguo kuchanika leo Juni 3, 2023 wakati wa bonanza la michezo la kujenga uhusiano baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe   Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP).

 Bonanza hilo ambalo ngeni rasmi alikuwa Mkuu wa Chuo hicho, Profess Hozen Mayaya lilishuhudiwa pia na Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Nicodemus Maganga limefanyika katika viwanja vya Shule ya John Merlin jijini Dodoma.

Michezo iliyoshindaniwa ni soka, Pete, mbio, kuvuta kamba, mbio za magunia na mchezo wa kufukuza kuku.

Kwa upande wa soka timu za Mbogwe na Mipango zilitoka sare ya mabao 2-2,  mbio walishinda Mbogwe, kuvuta kamba walishinda Mipango, mbio za magunia  Mbogwe, kufukuza kuku walishinda Mipango na Pete ushindi ulienda kwa watumishi wa Mipango kwa vikapu 18-15.
















 Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Viongozi wakielezea kuhusu bonanza hilo...IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana