Featured

    Featured Posts

AWESO AWAOMBA MSAMAHA WANANCHI WALIOCHELEWESHEWA MRADI WA MAJI.

 


SIKU  chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo kumuagiza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwenda kushughulikia tatizo la Mradi wa Maji wa Kata ya Uhambingeto katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Aweso amefika kwenye mradi huo na kuwaomba msamaha wanaanchi hao..


Aweso amekiri kuwa kuna uzembe ulifanyika kwenye utekelezaji wa mradi huo na kwamba ndio sababu ya kukwama na akaahidi kuukamilisha mradi huo ndani ya miezi mitatu ili tatizo la uhaba wa maji kwenye eneo hilo liishe.


Amewataka watendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) pamoja na viongozi wa Mkoa wa Iringa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kila wiki..


Katika hatua nyingine,Aweso amewaomba wananchi wa eneo hilo kuwa wavumilivu wakati Wizara yake inaendelea kukamilisha mradi huo.




author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana