Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MWINYI AENDA UJERUMANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka jana Zanzibar Juni 15, 2023 kwenda Ujerumani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu (Special Olympics World Games) ambayo maelfu ya wanamichezo wenye mahitaji maalumu kushindana katika michezo mbalimbali, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe: 17 hadi 25 Juni 2023


Rais Dk. Mwinyi katika safari hiyo ameambatana na  Waziri wa Habari Vijana na Michezo Mhe. Tabia Mwita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Mbarouk Nassor  Mbarouk pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 


Mbali na kushiriki uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu jijini Berlin, Rais Dk, Mwinyi pia atakutana na viongozi wa juu wa Serikali nchini humo, Wakuu wa Mashirika mbalimbali, Wawekezaji na jamii ya Watanzania waishio Ujerumani (Diaspora).



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana