Featured

    Featured Posts

RC BABU: KABLA YA 2024 SAME MWANGA UHABA WA MAJI UTAMALIZIKA

Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu  amewakikishia wakazi wa Wilaya za  Same na Mwanga kuwa tatizo la uhaba wa Maji litamalizika kabla ya Mwaka 2024 utakapokamilika Mradi mkubwa wa Maji Same, Mwanga-Korogwe.


Mkuu wa Mkoa aliyasena hayo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya wilayani Same na kuwataka Madiwani wa Halmashauri hiyo  kueneza taarifa hizo kwa Wananchi waweze kufahamu hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassani.


 "Mama yetu Mhe.Rais Samia Suluhu Hassani ametoa fedha nyingi kuakikisha Mradi huu Mkubwa wa Same Mwanga korogwe unakamika kwa wakati kuwawezesha wananchi  kunufahika na Mradi huo".Alisema Mkuu wa Mkoa.


Aidha alisema, kazi kubwa ya Madiwani ni kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani Katika utekelezaji wa Miradi na kuwaelimisha wananchi kufaham faida ya Miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.



Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mkoa . amewataka Madiwani kushirikiana kikamilifu katika kutoa Elimu kwa wananchi na pia kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani katika kuleta maendeleo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana