Featured

    Featured Posts

CHINGOLO APAMBANIA KERO ZA WANANCHI KUPATA SULUHISHO KONDOA

Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Daniel Chongolo akikaribishwa na wanachama wa chama hicho alipowasili kushiriki kikao Cha Shina namba 6 Itaswi Juni 19,2023 wakati wa ziara yake ya siku 8 katika Jimbo la Kondoa Vijijini,mkoani wa Dodoma.

Katika kikao hicho, Chongolo akisikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo ujenzi wa bwawa kwa ajili ya maji ambapo aliagiza ujenzi wake uanze Juni 10, 2023, kuwapelekea umeme ambapo meneja wa Kanda wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), akiahidi kuwa jambo Hilo litakamilika Desemba mwaka huu.

Aidha, ameiagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa anaharakisha ulipaji fidia  kwa walioathirika kwa namna moja ama nyingine na wanyamapori wanaotoka hifadhi ya Mkungunero.


Katibu wa NEC Oganaizesheni wa CCM, Issa Haji Gavu akiwasalimia wanachama na wananchi.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema akihutubia katika kikao hicho kwa kuwataka Wazazi kuwapeleka Shule watoto wa kike badala ya kuwaozesha na kuwatafutia ajira za majumbani.

 Mwenyekiti wa Shina namba 6 Itaswi Kondoa Vijijini, Msafiri Steven akifunga kikao hicho. Kulia ni Komredi Chongolo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana