Featured

    Featured Posts

UWT DAR YAWAFUNDA VIONGOZI, MWENYEKITI MWAJABU AWAKUMBUSHA KUYASEMA MAZURI YANAYOFANYWA NA RAIS SAMIA

Na CCM Blog, Dar
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Mwajabu Mbwambo amewafunda Viongozi na Watendaji UWT ngazi zote na kuwahimiza kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Aliwahimiza kila wanapozungumza na makundi kuhakikisha wanajenga hoja na kujibu hoja kwa hoja bila kutumia lugha zenye ukakasi, na kuwafunda kuwa pia kuwa ili waweze kufanya hivyo lazima Wajiamini huku wakisimama vyema katika nafasi zao.

Mwenyekiti Mwajabu ametoa darsa hilo wakati akitoa mada kwenye mafunzo kwa Viongozi na Watendaji wa UWT ngazi ya mkoa, Wilaya na Kata, yaliyoendeshwa na Kamati ya Utekelezaji UWT mkoa  huo, ikiongozwa na yeye (Mwajabu), juzi.

Katika kuwafunda, Mwenyekiti Mwajabu aliwahimiza Wanawake kwenda kutekeleza waliyofunzwa katika mafunzo hayo ili kubadilika katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Miongo mwa Mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ni Majukumu ya viongozi na watendaji wa UWT, Maadili ya viongozi na watendaji, Itifaki kwa viongozi, Siasa na Uchumi, Utambuzi wa Sheria na Haki za Wanawake na watoto, ukatili wa kijinsia na Afya ya akili na kudhibiti mihemko ya viongozi na watendaji.

Mapema mgeni katika mafunzo hayo, rasmi Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Adam Ngalawa ambaye pia ni Mjumbe wa Hamlashauri Kuu ya CCM Mkoa Dar es Salaam, alikumbusha kuwa Washiriki kuwa UWT ndio Jeshi la ushindi wa CCM, hivyo wasibweteke.

Aliwasihi Viongozi na watendaji UWT lazima watambue majukumu yao na kutenda kazi zao kwa ufanisi na weledi na kuwahamasisha kuwa na mkakati wa kushawishi na kuongeza wanachama wapya katika Jumuiya hiyo.

Ngalawa aliwahimiza kuwa mstari wa mbele katika kubaini changamoto zinazowakabili  Wanawake na watoto na kuzitafutia utatuzi kila nyakati.

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Mwajabu Mbwabo akitoa darsa wakati akiwasilisha mada kwenye mafunzo kwa Viongozi na Watendaji wa UWT ngazi ya mkoa, Wilaya na Kata, yaliyoendeshwa na Kamati ya Utekelezaji UWT mkoa huo, ikiongozwa na yeye, juzi.
Mgeni rasmi Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Adam Ngalawa akizungumza kwenye mafunzo hayo. Ngalawa pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa huo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wasiriki wakimsikiliza Mwenyekiti Mwajabu wakati akiwasilisha mada. (Picha na Habari kwa Hisani ya Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Mwajabu Mbwambo).
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana