Featured

    Featured Posts

CHONGOLO AFURAHISHWA NA MRADI MKUBWA WA BWAWA NSENKWA WILAYANI MLELE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi Daniel Godfrey Chongolo akisalimiana na Chifu wa Kabila la Wakonongo, mwenye utawala wa eneo la Kalovya, Chifu Michael Kayamba, leo Jumatano Oktoba 5, 2023, baada ya Ndugu Chongolo kuwasili Jimbo la Katavi, wilayani Mlele, kutembelea na kukagua mradi mkubwa wa Bwawa la Nsenkwa, linalojengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji safi na salama kwa matumizi ya wananchi wa vijiji 16 katika Halmashauri ya Mlele mkoa wa Katavi. Mradi huo utakaowahudumia takribani wakazi 68,000 utagharimu jumla ya Sh. 2.8 bilioni. 

Akiwa katika eneo hilo la mradi, Katibu Mkuu Komredi Chongolo, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo kutoka kwa Watendaji wa Wizara ya Maji, Ruwasa, Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mlele, waliobuni mradi huo, aliwapongeza kwa kubuni jambo litakalokuwa na matokeo makubwa na chanya kwa wananchi, kwa gharama ndogo.

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Daniel Chongolo (kushoto) akikagua Bwawa la maji safi la Nsenkwa, wilayani Mlele mkoani Katavi Oktoba 5, 2023 wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo. Kulia ni Katibu wa NEC-Oganaizesheni, Haji Issa Gavu.

Bwawa hilo litakalohudumia vijiji 16, zaidi ya watu 68,000 limejengwa kwa gharama ya sh. Bil. 2.8.

Chongo amechangia sh. 500,000 za kununua vifaranga vya samaki kwa ajili ya kupandikiza kwenye bwawa hilo. Pia ameutaka uongozi wa Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele kuchangia sh. Mil. 1-5 za kununua vifaranga kwa ajili ya kupandikiza kwenye bwawa hilo.

Mbunge wa Katavi, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga. 

Chongolo akizungumza na wananchi wa eneo hilo.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Mlele, Charles Mengo akisoma taarifa ya mradi huo.
Mbunge wa Katavi, Isack Kamwelwe akitoa shukrani kwa Komredi Chongolo kukagua mradi huo lakini shukrani zilenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kugharamia mradi huo.
Chifu Michael Kayamba wa Kabila la Wakonongo Kalovya akitoa shukrani kwa serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa bwawa hilo.
Komredi Chongolo akizungumza  na wananchi baada ya kukagyua bwawa hilo ambapo pia alichangia sh. 500,000 za kununulia viranga vya samaki kwa ajili ya kupandikiza kwenye bwawa hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga akionesha sh. 500,000 zilizotolewa na Chongolo kwa ajili ya kununulia vifaranga hivyo
Baadhi ya wananchi wa eneo la Nsenkwa wakisikiliza kwa makini wakati Chongolo akizungumza nao.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana