Featured

    Featured Posts

TASAC: USIKIVU WA RAIS DK. SAMIA UMETUVUSHA KUCHANGIA KATIKA MFUKO MKUU WA SERIKALI KUTOKA SH. BILIONI 9.1 HADI KUFIKIA BILIONI 43.49

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limesema, usikivu wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akipokea ushauri wa kitaalamu na ushauri na miongozo kutoka Kamati za Bunge, umeiwezesha TASAC  ongezeko la mchango wake katika mfuko mkuu wa Serikali kutoka sh. Bilioni 9.1 mwaka 2018/19 hadi kufikia sh. Bilioni 43.49, mwaka 2021/22.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali, kwenye kikao kazi baina ya Wahariri, Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na TASAC, chini ya uratibu wa  Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 5, 2023.

Akieleza mafanikio wakati akitoa taarifa ya Utendaji kazi wa TASAC, Mlali alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kuongeza idadi ya kadhia zilizohudumiwa kutoka 6,000 mwaka 2019/20 hadi zaidi ya kadhia 10,000 mwaka 2021/22.

Mafanikio mengine aliyataja kuwa ni kuunda nyenzo za udhibiti wa usafiri majini ikiwa ni pamoja na kanuni na miongozo kuwezesha utekelezaji wa sheria katika kudhibiti usafiri majini, kuongeza idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC kwa maana ya idadi ya leseni na vyeti vya usajili vilivyotolewa na kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti, kuongezeka kwa idadi ya leseni za vyombo vidogo na kuongezeka kwa idadi ya kaguzi za meli za kigeni.

Kwa upande wa Wahariri, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kwa kuweka utaratibu wa Mashirika ya Umma kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kueleza utekelezaji wa majukumu yao.

Alisema, kupitia vyombo hivyo vya habari umma umekuwa ukipata fursa ya kufahamu shughuli mbalimbai zinazotekelezwa na mashirika hayo. "Kwa mfano bila mkutano huu ulioandaliwa na TR, ingechukua muda mrefu kujulikana kuwa TASAC imechangia kutoka sh. Bilioni 9.1 mwaka 2018/19 hadi kufikia sh. Bilioni 43.49, mwaka 2021/22 katika Mfuko Mkuu wa Serikali", akasema Balile.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali (kushoto), akipongezwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) Eric Mkuti, baada ya kuwasilisha taarifa ya Utendaji wa TASAC, kwenye kikao kazi baina ya Wahariri, Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na TASAC, chini ya uratibu wa  Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 5, 2023.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Utendaji wa TASAC, kwenye kikao kazi baina ya Wahariri, Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na TASAC, chini ya uratibu wa  Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 5, 2023.
Washiriki wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Utendaji wa TASAC, kwenye kikao kazi baina ya Wahariri, Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na TASAC, chini ya uratibu wa  Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 5, 2023.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali, akiwa ameketi kusubiri maswali baada ya kuwasilisha taarifa ya Utendaji wa TASAC, kwenye kikao kazi baina ya Wahariri, Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na TASAC, chini ya uratibu wa  Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 5, 2023.
Afisa Uhusiano na Mawasilino Ofisi ya Msajili wa Hazina  Sabato Kosuri akikaribisha washiriki kuuliza maswali. 

Baadhi ya Wahariri wakiuliza maswali👇

Salim kutoka Zanzibar
Jabir kutoka Zanzibar
Kulangwa
Kubenea.
Mzee Sadik

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali (kushoto), akinakili maswali. Kulia ni Mkut kutoka TR.
Kosuri akimwalika Mlali kujibu maswali.

Mlali akijibu maswali.
Kosuri akimualika Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile, kuzungumza.
Balile akizungumza.
Ofisa habari wa TASAC akizungumza.

Mlali akifunga kikao hicho. 

Ikafuatia Picha za pamoja👇

 ---------------------------------------------

Wasilisho lililotolewa na TASAC katika Kikao hicho👇

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana