Featured

    Featured Posts

CHONGOLO: NITAHAKIKISHA KITUO CHA AFYA, BARABARA MLIMA LYAMBA LYA MFIPA KUJENGWA

 

Katibu Mkuu wa CCM Komredi Daniel Chongolo akitoa Saini kwenye kitabu Cha wageni aliposhiriki katika kikao cha shina namba 9 Tawi la Kalakala, Kata ya Muze, Sumbawanga Vijijini Oktoba 10, 2023, wakati ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama ya 2020-2025.

Chongolo, ameahidi kwenda kusukuma serikali kupeleka haraka fedha za ujenzi wa Kituo Cha Afya na kuhakikisha ujenzi wa barabara inayopita Mlima Lyamba lya mfipa inayokwenda katika kata ya Muze Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga unaharakishwa.

Komredi Chongolo akiwa na Mwenyekiti wa Shina hilo, Salvatore Kasima.
Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM pamoja na wajumbe wa Shina hilo wakiwa katika kikao hicho.




Mwenyekiti wa Shina Kasima akifungua kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere akijitambulisha kwa wananchi. Kushoto ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia AAlly Chirukile.
Katibu wa NEC Oganaizesheni CCM,  Issa Haji Gavu akihutubia katika kikao hicho.Amewaahidi wanachama wa CCM wa eneo kuanza kupata kadi moya za kielektriniki.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana