Featured

    Featured Posts

NI KIMBUNGA MKUTANO WA CHONGOLO KWELA, SUMBAWANGA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Daniel Chongolo akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kaliamatundu, Jimbo la Kwela, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Rukwa Oktoba 10, 2023, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.

Katika mkutano huo Komredi Chongolo ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganaizesheni, Issa Haji Gavu amesisitiza wazazi kuwapeleka shule watototo wa kike ili wapate elimu ambayo ni urithi wao sahihi kuliko mali, kuboresha huduma za afya na hasa kwa wajawazito ili wawe wanajifungua salama hivyo kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi, vijiji vyote vipate umeme ifikapo Desemba 2023, usamabazaji maji vijiji pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.

Leo Komredi Chongolo atakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara mjini Sumbawanga kuzungumzia kwa ujumla yaliyojiri kwenye ziara yake hiyo ya Mkoa wa Rukwa ambao pia utahudhuriwa na baadhi ya mawaziri watakaojibu kero mbalimbali za wananchi wa mkoa huo.



Sehemu ya wananchi wakisikilia=za wakati Komredi Chongolo akihutubia



IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA


 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana