Featured

    Featured Posts

LATRA: MIONGOZO BORA YA RAIS DK. SAMIA IMETUPA KASI YA AJABU, TUNAJIENDESHA BILA RUZUKU, TUMECHANGIA MFUKO MKUU WA SERIKALI SH. BILIONI 14.21 NDAJI YA MIAKA MITATU

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) imesema kufuatia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuipa miongozo mizuri imepiga hatua kubwa kwa urahisi katika kuleta mapinduzi ya uhakika kwenye sekta ya usafiri wa ardhini nchini.

Imesema, sanjari na kupiga hatua hiyo, pia utendaji wa Mamlaka hiyo, umekuwa bora kiasi kwamba inajiendesha bila kupewa ruzuku na serikali, badala yake imekuwa ikitoa gawio la kutosha kwenye mfuko wa serikali, na haijawahi kupata hati chafu kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali CAG).

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA. Habibu Saluo, amesema. hayo kwenye kikao cha LATRA na Wahariri wa habari kwa lengo la kujenga ulelewa wa kina kuhusu utendaji wa Mamlaka hiyo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 19, 2023, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, (OTR).

“Mamlaka hupaswa kuchangia asilimia 15 ya mapato yake ghafi kwenda kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali (Consolidated Fund) kwa mujibu wa Kifungu cha 11(3) cha Sheria ya Fedha za Umma, Sura ya 348 (Public Finance Act, Cap. 348).

Mamlaka hutakiwa kuchangia asilimia 70 ya fedha za ziada (surplus funds) kila mwisho wa mwaka wa fedha kwenda katika Mfuko Mkuu wa Serikali kwa mujibu wa kifungu cha 42 cha Sheria ya Bajeti, Sura ya 439. Sasa Katika kipindi cha miaka mitatu, mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2022/23, Mamlaka imeweza kuchangia Sh. Bilioni 14.21 katika Mfuko Mkuu wa Serikali", amesema CPA. Saluo.

Kuhusu mapato, CPA Saulo, alisema, mapato ya Mamlaka ya LATRA yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka, akisema, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2021/22, mapato yaliongezeka kutoka Sh. Bilioni 25.945 hadi Sh. Bilioni 28.53, ikiwa ni ongezeko la Sh. Bilioni 2.58 sawa na ongezeko la asilimia 10.

Alisema, pia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 hadi 2022/23, mapato ya Mamlaka yaliongezeka kutoka Sh. Bilioni 28.53 hadi Sh. Bilioni 34.17 (kabla ya kukaguliwa na CAG) ikiwa ni ongezeko la Sh. Bilioni 5.64 sawa na ongezeko la asilimia 20.

“Kwa jumla, katika kipindi cha miaka mitatu (3) ya utekelezaji wa majukumu ya LATRA, mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2022/23, mapato ya Mamlaka yaliongezeka kutoka Sh. Bilioni 25.95 hadi Sh. Bilioni 34.17 (kabla ya kukaguliwa na CAG) ikiwa ni ongezeko la Sh. Bilioni 8.22 sawa na ongezeko la asilimia 32", alisema CPA Saulo.

Kuhusu leseni, CPA Saulo alisema, katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2022/23, idadi ya leseni za usafirishaji ziliongezeka kutoka 230,253 hadi 284,158 sawa na ongezeko la leseni 44,205 ambayo ni ongezeko la asilimia 18.4.

CPA Saulo alisisitiza kwamba, pamoja na matumizi ya TEHAMA ilikojikita LATRA katika utoaji huduma, juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita zimechangia sanakubwa kuongezeka kwa ufanisi wa utoaji huduma.

“Serikali imeboresha miundombinu ya barabara kila kona zikiwemo zile njia zinazolisha njia kuu (feeder roads), hali ambayo imewezesha kuwavutia watoa huduma kuwekeza kwenye biashara ya usafirishaji. Kwa dhati kabisa tunaishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama yetu Rais Dk. Samia", Alisema CPA. Saluo.

Akitoa utangulizi kabla ya kumualika CPA Saulo kuwasilisha taarifa ya LATRA, Afisa Uhusiano Mwandamizi katika Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, alisema, Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), inasimamia Mashirika ya Umma, Taasisi za Umma na Kampuni ambazo serikali ina umiliki wa zaidi ya asimlimia 30.

Kosuri alisema, lengo la Ofisi ya Msajili wa Hazina ni kuona, Taasisi, Mashirika na Kampuni hizo zinafikia malengo ya kuanzishwa kwake na kushajihisha kuwa kiasi kikubwa mashirika hayo yamefikia malengo kwa kiwango cha kuridhisha ingawa machache bado hayajafikia.

Alisema serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia, imeona ifanye mageuzi na mapinduzi makubwa ndani ya Mashirika, Taasisi na Kampuni hizo kwa nia ya kuonegza tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi na pia kuliingizia taifa kipato.

“Kwa hiyo Ofisi ya Msajili wa hazina imeeleekeza Taasisi, Mashirika na kampuni hizi, kupitia ninyi Wahariri wa habari yaeleze umma ni kwa kiasi gani wamefanikiwa kufikia malengo ya kuanzishwa kwake”, akasema Kosuri.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Mjumbe wa Jukwaa hilo, Nevile Meena, aliishukuru Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kuratibu utaratibu huo wa Wahariri kukaa na viongozi wa Taasisi, Mashirika na Kampuni zilizopo chini ya Serikali kwa lengo la kufikishia umma hali halisi ya utendaji.

Pia Meena, aliishukuru LATRA kwa kutika wito Ofisi ya Msajili wa Hazina, lakini pia kwa kutoa kinagaubaga mbele ya wahariri hao maelezo 'yaliyoshiba' na kujibu kwa usahihi maswali waliyoulizwa LATRA hao.

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) CPA Habibu Saluo, akizungumza kwenye kikao cha LATRA na Wahariri wa habari kwa lengo la kujenga ulelewa wa kina kuhusu utendaji wa Mamlaka hiyo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 19, 2023, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, (OTR).
Afisa Uhusiano Mwandamizi katika Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, alipokuwa akitoa utangulizi,kabla ya kumualika CPA Saulo kuwasilisha taarifa ya LATRA, kwenye kikao hicho.
Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa habari wakiwa kwenye kikao hicho.
CPA Saulo akiendelea kuzungumza kwenye kikao hicho.

Wahariri na waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini CPA Saulo.

CPA Saulo akijibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri katika kikao hicho. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Usafiri Wa Reli, Mhandisi Hanya Mbawala.


Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Nevil Meena akizungumza mwishoni wa kikao hicho.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari-LATRA, Salum Pazi, akizungumza mwishoni mwa kikao hicho.
 

IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI YA LATRA KAMA ILIVYOWASILISHWA NA CPA SAULO KWENYE KIKAO HICHO👇

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana