HISTORIA YA JIMBO AICT KITANGILI -DAYOSISI YA SHINYANGA
Viongozi wandamizi Kanisa la AIC Jimbo la Kitangili Shinyanga |
Mnamo Septemba 08-10, 2021 Baraza la Sinodi kuu,Buzuruga,Mwanza lilipitisha Katiba iliyorekebishwa kukubali mabadiliko ya kiuendeshaji ikiwemo Kubadili jina la ngazi ya Chalo kuwa Jimbo basi,mnamo tarehe 14/05/2022 ndipo Jimbo la AICT Kitangili likanzishwa likiwa na Pastoreti 12, Wachungaji 13, Wainjilisti 53 na Kanisa za mtaa 53.kama ifuatavyo
- Pastoreti 8 zimo katika Manispaa ya Shinyanga ambazo ni: Kambarage,Mlima Betheli -Kitangili,Ndala,Nhelegani,Giligali – Ngokolo, Samaria-Bugweto,Chibe na Old Shinyanga.
- Pastoreti 2 zimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambazo ni: Mishepo na Usule.
- Pastoreti 2 zimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambazo ni: Bethelehemu- Bunambiyu na Bulima.
BARAZA LA KWANZA LA JIMBO
Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Zakayo E.Bugota mnamo tarehe 14/05/2023 alisimamia Baraza la kwanza la Jimbo AICT Ktangili kufanya mambo yafuatayo
Kuchagua viongozi Wandamizi wa Jimbo kama ifuatavyo:
- Mchungaji Paul Makenzi Kidanha kuwa Mchungaji Mwenyekiti wa Jimbo
- Mchungaji Joshua S.Masaga kuwa Mchungaji Mwenyekiti Msaidizi wa Jimbo.
- Mwalimu Samwel Lazaro Maziku kuwa Kaimu Katibu wa Jimbo na
- Mwinjilisti Anna Charles Lugenji kuwa Kaimu Mhasibu wa Jimbo.
Viongozi wandamizi wakisimikwa 14/05/2023 |
Kuamua kuwa Makao Makuu ya Jimbo la Kitangili yawe Pastoreti ya Mlima Betheli-Kitangili.
Sherehe ya kuwapongeza viongozi wapya wa AICT Jimbo la Kitangili Shinyanga |
Ibada Maalumu ya uzinduzi wa Jimbo la AICT KITANGILI ilifanyika Oktoba 15 Jumapili 2023 ikiongozwa na Baba Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota kwa:-
- Kuzindua Jimbo
- Kusimika viongozi wandamizi wa Jimbo na
- Kusimamia mchango wa Ujenzi wa ofisi za Jimbo
Post a Comment