Featured

    Featured Posts

MAKONDA MWENEZI MPYA CCM, RABIA KUSHIKA SUKI, NEC YAIELEKEZA SERIKALI KUENDELEA HATUA YA KUSAINI MIKATABA UWEKEZAJI BANDARI

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi, kuchukua nafasi ya Sophia Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Wanawake, watoto na Makundi Maalum.

CCM imemteua Makonda katika Kikao chake cha NEC, kilichofanyika Mjini Dodoma, leo Oktoba 22, 2023, chini ya Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho pia kimemteua Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), kuchukua nafasi ya  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi imesema, pamoja na hayo Kikao hicho cha NEC ambacho kilikuwa maalum kimeridhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa bandari.

Aidha katika Kikao hicho NEC, imezipongeza Serikali zake zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. Samia suluhu Hassan na ya Mapinduzi Zanzibar Rais Dk. Hussein Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-25.

Paul Makonda

 TAARIFA RASMI YA CCM👇



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana