Featured

    Featured Posts

MWENEZI CCM TAWI LA DMV MAREKANI SALMA MOSHI AMPONGEZA MAKONDA

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Naoibduzi ( CCM) tawi la Washington DC  Virginia na Maryland (DMV) Salma Moshi amempongeza Paul Makonda kwa kuteuliwa na CCM kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.


Katika salamu alizozituma kupitia Blog ya Taifa ya CCM, Salma amesema ana matumaini kwamba Makonda ataleta chachu kubwa katika chama kwa kuwa ni mhapakazi.


"Kwa niaba yangu na wanachama wa CCM tawi la DMV nampongeza Ndugu Makonda kwa kuteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, mimi na wenzangu tunaamini ataleta chachu kubwa katika Chana. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI", amesema Salma katika salam hizo.

Makonda ameteuliwa kuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, katika Kikao cha NEC kilichofanyika mjini Dodoma leo Oktoba 22, 2023 chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Salma Moshi akiwa na Makonda, siku zilizopita.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana