Featured

    Featured Posts

MJEMA KUWEKA MSUKUMO UJENZI KITUO CHA AFYA MAJALIWA

 




 Nachingwea, LINDI


Jumatatu Oktoba 16, 2023

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Ndg. Sophia Mjema, ametembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kassim Majaliwa ( jengo la wagonjwa wa nje) kilichopo kata ya Chiola, Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Lindi.

Mradi huo wa ujenzi wa jengo la OPD umeanzishwa kwa nguvu za wananchi ambapo mpaka sasa wameshachangia sh. milioni 38.8 mpaka hatua ya lenta. Hadi mradi kukamilika unakadiriwa kugharimu sh.milioni 193.4.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg. Sophia Mjema, ameahidi kuwasiliana na Waziri wa TAMISEMI, kuona fedha zinapatikana kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa kituo hicho.


Halmashauri ya Nachingwea imeandika barua kwenda  TAMISEMI kwa ajili ya umaliziaji wa mradi huo.


#CCMIMETIMIA

#KAZIIENDELEE

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana