Featured

    Featured Posts

TIB: TUNACHAPA KAZI KWA WELEDI ILI KUFIKIA AZIMA YA SERIKALI CHINI YA RAIS DK. SAMIA KUIFUNGUA NCHI KATIKA UCHUMI WA DUNIA, YAWEKEZA BILIONI 980/- KWENYE MIRADI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
BENKI ya Maendeleo ya TIB imesema inatekeleza majukumu yake kwa weledi ili kufikia azma ya Serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ya kuifungua nchi katika uchumi wa Dunia kupitia kuboresha mazingira ya uwekezaji, uendelezaji miundombinu mikubwa kuharakisha mtiririko mzuri wa Uwekezaji wa moja kwa moja wa Nje(FDI)  na uwekezaji wa moja kwa moja wa Ndani(DDI)  kwa jamii na ustawi wa uchumi wa taifa.

Imesema katika kufanya hivyo kwa welesi benki hiyo imefanikiwa kulifungua Taifa kwa kufanya uwekezaji wenye tija kiasi cha kufanikiwa kuwekeza hadi Sh. bilioni 334.7 kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo nchini na pia kufanikiwa kufanya uwekezaji kwenye sekta ya nishati, maji.

Hayo yamesemwa  na Kaimu Mkurugenzo wa TIB  Lilian Mbassy, akizungumza katika kikao na Wahariri wa habari kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16, 2023, kwa uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), na kufafanua kuwa hadi kufikia Septemba 30, 2023, benki hiyo imewekeza kwenye miradi ya jumla ya Sh. Bilioni 980.7.

Alifafanua kuwa katika uwekezaji huo asilimia 93 ya miradi hiyo ni ya sekta binafsi na asilimia 7 ni ya sekta ya umma huku asilimia 80 ya miradi ikiwa ni ya muda mrefu wa zaidi ya miaka mitano.

Lilian amesema, chachu ya TIB kupata mafanikio ni mikakati yake madhubuti ya kuhakikisha benki hiyo inatoa huduma bora kwa umma na sekta binafsi, lakini kubwa zaidi ni 'sapoti' ya ruzuku ambayo wamekuwa wakipewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk, Samia Suluhu Hassan, huku akiweka bayana kwambaTIB haifanyi kiholela uwekezaji kwenye miradi bali ni kwa kuzingatia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa.

Kaimu Mkurigenzi wa Benki ya Maendeleo -TIB Lilian Mbassy, akizungumza katika kikao na Wahariri wa habari kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16, 2023, kwa uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR).

TAARIFA YOTE ILIYOWASILISHWA NA KAIMU MKURUGENZI TIB LILIAN MBASSY HII HAPA👇
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana