Featured

    Featured Posts

SEKONDARI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 2006 YAAMUA KUANZA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI*



Nyanja Sekondari ni ya Kata ya Bwasi yenye vijiji vitatu (3) vyenye jumla ya vitongoji ishirini na vitatu (23). Vijiji hivyo ni Bugunda, Bwasi na Bugunda.


Sekondari hii ilifunguliwa Mwaka 2006, na kwa sasa ina jumla  ya wanafunzi 547, na walimu 12 wenye ajira, na 5 wa kujitolea.


*Harambee ya ujenzi wa maabara:*

Sekondari haina maabara hata moja na mwitikio wa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ni mdogo sana


Kwa mfano, Kidato cha Nne (Form IV) chenye jumla ya wanafunzi 96, ni wanafunzi 13 tu wanaosoma somo la Fizikia.


*Jana, Jumatatu, 9.10.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) waliendesha HARAMBEE ya kuanza ujenzi wa maabara za Fizikia, Kemia na Baiolojia za sekondari hiyo.


*Mapato ya Harambee:*

*Fedha: Tsh 1,105,000

*Saruji Mifuko 141

(ikiwemo Mifuko 100 ya Mbunge wa Jimbo)


*Kamati ya Ujenzi:*

Kamati ya Ujenzi ya watu wanne (4) imeundwa.


*KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA KATA ZA MUSOMA VIJIJINI*


Idadi ya Sekondari Jimboni (Kata 21) mwetu:

*25 za Kata

*2 za Binafsi

*5 zinajengwa


Picha za hapa zimechukuliwa kwenye Harambee ya jana iliyofanyika Nyanja Sekondari, Kijijini Kome, Kata ya Bwasi


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

https://ift.tt/JztYj62 


Tarehe:

Jumanne, 10.10.2023

 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana