Featured

    Featured Posts

WCF YAWAHAKIKISHIA HUDUMA BORA WATEJA WAKE

NA K-VIS BLOG, DODOMA
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma,  amewataka wafanyakazi wa Mfuko huo kudumisha Ushirikiano ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama na wadau wa Mfuko wakiwemo waajiri, wanufaika na wafanyakazi pale watakapopata ajali ama kuugua kutokana na kazi.

Dkt. Mduma ameyasema hayo Oktoba 4, 2023 kwenye ofisi za WCF, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya WCF ya wiki ya Kimataifa ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 2, 2023.

Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja ni tukio la kimataifa ambalo linaangazia umuhimu wa huduma kwa wateja na watu wanaotoa huduma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kwa watoa huduma na wateja, ambapo mwaka huu wa 2023 imebeba kaulimbiu ya “Ushirikiano kwa Huduma Bora.”

“WCF chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu tumekuwa tukifanya kazi na kutoa huduma kwa ushirikiano kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema, kuanzia ngazi ya mkurugenzi mkuu, Menejimenti mpaka kwa afisa wa kawaida.” Amesema na kuongeza..  Katika maisha yetu tunafurahia kufanya kazi na kutoa huduma kwa pamoja   tena kwa ushirikiano mkubwa bila kujali yupi ni wa ngazi ipi.” Amesisitiza Mkurugenzi Mkuu.

Amesema kama ilivyo desturi ya wafanyakazi wa WCF, kwa kauli mbiu ya mwaka huu “TEAM SERVICE” au HUDUMA KWA USHIRIKIANO, inakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa kutambua ushirikiano ambao utawezesha kutoa huduma bora zaidi kwa wateja na wadau bila kusubiri wale walio katika madawati ya mapokezi.

Katika ofisi za WCF za Dar es Salaam, Temeke, Ilala, Arusha, Mbeya, Mwanza, Geita na Morogoro, wakuu wa ofisi hizo wamewahimiza wafanyakazi wenzao kuhakikisha wanadumisha ushirikiano baina yao wenyewe lakini na wanaowahudumia ili kudumisha taswira nzuri iliyopo ya Mfuko huo.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma,  akimuhudumia mteja (Mwnaachama) wa Mfuko huo kwenye ofisi za WCF, jijini Dodoma Oktoba 4, 2023.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana