Featured

    Featured Posts

MKUTANO WA IDA 20 KUWAKUTANISHA ZANZIBAR WAJUMBE 300 KUTOKA MATAIFA 100, RAIS DK. MWINYI AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA YA UGENI HUO

Zanzibar
Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid-Term Review) utakaofanyika Zanzibar, kuanzia tarehe 6 hadi 8 Disemba 6-8, 2023, uunatarajiwa kuwashirikisha wajumbe zaidi ya 300 kutoka mataifa takribani 100 duniani.

Akihojiwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha Benny Mwaipaja, kuhusu Mkutano huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewakaribisha washiriki wa mkutano huo nchini Tanzania hususan, katika Visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar), kushuhudia Maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii yaliyofikiwa kutokana na mikopo nafuu na misaada kupitia Benki ya Dunia.

Rais Dk. Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa za ugeni huo katika Sekta mbalimbali ikiwemo utalii, wakati wa Mkutano huo wa siku tatu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, akihojiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha Benny Mwaipaja, kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid-Term Review), Ikulu mjini Zanzibar, leo.
 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana