Featured

    Featured Posts

MUASISI CHAMA CHA CCK AMPONGEZA MAKONDA, ASEMA ANASIMAMIA VEMA KUHAKIKISHA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM INATEKELEZWA

Hizi ni salamu za upendo na pongezi kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Ndugu Paul Makonda kwa kuteuliwa na kuanza kazi kwa kishindo kikubwa.

Tanzania kwa sasa inashuhudia kiongozi mpya, Paul Makonda, ambaye ameanza majukumu yake kama Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM kwa kishindo kikubwa. 

Kwa ujasiri na kujitolea, ametoa matamko makali kwa viongozi wa serikali, akilenga kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii ili kuleta ufanisi na uwajibikaji katika serikali. 

Tumeshuhudia akiwaagiza Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote nchini kujipanga ili kuondosha kero zinazowasumbua wananchi na kwamba kwa upande wa Mawaziri wawasilishe  ripoti ya utendaji wao kwa chama kila baada ya miezi mitatu, kutoa maelezo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Wako watu wameibuka wakimshambulia kiongozi huyu hadharani na kumbeza eti kwamba hana mamlaka hayo,

Nataka kuwakumbusha jambo moja tu, nalo ni kwamba, Makonda ametumwa na CCM, kukisemea chama chake yale waliyokubaliana kwenye vikao vyao.

Kushuhudia kiongozi wa CCM akichukua hatua za dhati za kuwajibisha viongozi wa serikali ni hatua muhimu kuelekea kujenga serikali bora na kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.

Paul Makonda ameonyesha utayari wake wa kusimamia dhamana ya chama kwa ujasiri na dhamira. Binafsi, nampongeza, kwa kukubali kutimiza majukumu yake bila woga wala hofu, kwa kufanya hivyo, anatii kiu ya Watanzania wengi wanaotaka kuona kwa vitendo chama kikishika hatamu katika kuiongoza serikali kwa maneno na vitendo, hali ambayo kwa muda mrefu inaonekana kupungua kutoka kwenye upande wa chama.

Amesimama kwenye nafasi yake na kupaza sauti ili kila kiongozi achukue majukumu yake kwa uzito unaostahili na kuwajibika mbele ya wananchi kupitia chama chake.

Ni muhimu kutambua kuwa katika mfumo wa kidemokrasia kama wa Tanzania, serikali inaundwa kwa ridhaa ya wananchi wakati wa uchaguzi. Kwa sasa, CCM ndiyo chama kilichounda serikali, na hivyo kinabeba jukumu kubwa la kuisimamia na kuhakikisha utekelezaji wa Ilani iliyowasilishwa kwa wananchi mnamo 2020. 

Kwa hivyo, hatua za Paul Makonda zinazingatia jukumu hili kikatiba la chama kuiongoza serikali isimamie mkataba wa wananchi na chama, yaani Ilani.

Wakati kuna wakosoaji wanaopendekeza kuwa nafasi yake kama Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi ya CCM haipaswi kuingilia mambo ya serikali, ni muhimu kuelewa kuwa jukumu la chama ni kusimamia serikali na kuhakikisha utekelezaji wa ahadi kwa wananchi. 

Paul Makonda amekumbusha viongozi wote wa serikali kuhusu wajibu wao na kuwa dira, katika kufika maelengo ya kimaendeleo, amewakumbusha kuhusu kuwajibika.

Nina ungana kwa dhati na Paul Makonda na kumtia moyo katika juhudi zake za kuendeleza dhamira ya CCM ya kuleta maendeleo na kuwatumikia wananchi. 

Kiongozi mwenye ujasiri na dhamira ya kuleta mabadiliko ni hazina kwa chama chake na taifa. Nina muunga mkono kwa nguvu na kumpongeza kwa kuanza kazi yake kwa dhamira ya kujitoa muhanga, huku nikiamini kuwa ujasiri wake utasaidia kuleta mabadiliko mazuri katika serikali na kuimarisha utumishi wa umma kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Nina muombea mafanikio katika majukumu yake kama Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi ya CCM. Ahsante kwa kujitolea kwa dhati katika kuleta mabadiliko na kuimarisha uongozi wa CCM.

Constantine Akitanda
Mtanzania,
Mtaalamu wa Siasa na Mawasiliano kwa Umma na Muasisi wa Chama Cha Kijamii (CCK)
Tarehe 03/11/2023

Katibu wa NEC, Itiadi na Uenezi Paul makonda.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana